Baada ya uhalali wa mtoto wa Mwimbaji wa nyimbo za injili Nchini Flora Mbasha kutawala kwenye magazeti mbalimbali na mitandao ya kijamii, hatimaye jipu limepasuka baada ya baba mdogo wa Flora aliyejitambulisha kwa jina moja la Kisekwa kufunguka kwamba mtoto huyo ni damu halali ya Mbasha.
NI MAHAKAMA YA ILALA
Kisekwa alifunguka hayo juzikati katika Mahakama ya Ilala Jijini Dar es Salaama alipokuwa amekwenda kusikiliza kesi ya aliyekuwa mume wa Flora, Emmanuel Mbasha kudaiwa kumbaka shemeji yake ambapo alisema anamshangaa Mbasha kushindwa kukiri ukweli ulio wazi kwamba mtoto ni damu yake wakati moyoni anautambua.
TUJIUNGE NA KISEKWA
"... Inakuaje Mbasha anashindwa kukubali ukweli kwamba mtoto ni wake wakati anatambua fika kwamba ujauzito ni mali yake kabla hata ya mgogoro wao? Ndugu wote tulikuwa tunajua hilo, upande wetu na kwao, mbona hakuikataa tangu kipindi hicho? mgogoro wao ulikuwa wa mambo ya kawaida ya kifamilia, haukuhusiana hata kidogo na flora kuchepuka wala nini, tangu mwanzoni mwa mgogoro wao wakiwa wanaishi pamoja wameshaitwa mara tatu katika ofisi za ustawi wa jamii na alielezwa kuwa mkewe ni mjamzito, akifahamu ni mali yake na akaonywa kuwa kitendo cha kuendekeza migogoro ya mara kwa mara kinaweza kumletea matatizo mkewe na kichanga kilichokuwa tumboni, mbona hakubisha?
tulikuwa tukijadili mtatizo yao na kila mmoja kuweka hoja zake mezani, hakuna kati yao aliyehusisha mgogoro huo na swala la kuchepuka.
KIAPO CHATAJWA
Kama hiyo haitoshi, kuonesha ana uhakika na anachokizungumza, Kisekwa alimtaka Mbasha ajiapize kwa kushika kitabu kitakatifu cha biblia kama ana mashaka na anachokizungumza.
AKERWA NA MADAI YA GWAJIMA
Mzazi huyo alisema kuwa anakerwa zaidi jinsi ambavyo Mbasha amewahi kukaririwa akimhusisha mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchungaji kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima kwamba ni baba wa mtoto huyo.
"... Anamsingizia tu baba wa watu (Gwajima) masikini ya Mungu kwa vile hapendi kuona anavyomsaidia Flora, lakini ukweli sisi Gwajima ni ndugu yetu, mimi G anniita baba mdogo kama anavyoniita Flora..." alisema Kisekwa.
MBASHA ANASEMAJE?
Wanaharakati wetu walipomtafuta Mbasha kuhusiana na ukweli kwamba kichanga ni mali yake, hakutaka kukubali wala kukataa zaidi ya kupinga ujomba wa Flora na Gwajima.
"... Flora aseme ukweli, ujomba wa yeye na Gwajima umetoka wapi? Hilo tu ndo nataka alifafanue kwa undani maana wajomba zake wote mimi nilitambulishwa wakati ninamuoa..." alisema Mbasha.
Mwandishi: Kuhusu ukweli kwamba mtoto ni wako, unalizungumziaje?
Mbasha: hilo litajulikana tu lakini mimi nataka kujua ujomba wake na Gwajima umetoka wapi? hapo tu..."
TUJIKUMBUSHE
Mbasha na Flora ambao waliishi kwenye ndoa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, mwaka jana walifikia hatua ya kutengana na kila mmoja kuishi kivyake baada ya kushindwa kutatua mgogoro wao wa muda mrefu wa kifamilia.
Endelea kufuatilia modesigntz Beste wangu wa ukweli, na mimi ntendelea kukusogezea kila stori inyonifikia...
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU ILI NAAWE UWE MWANFAMILIA NA HABARI ZETU ZIKUFIKIE MOJA KWA MOJA
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN



Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.