Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

BABA WA DIAMOND AMFAGILI MKWEWE ZARI KULIKO AKINA WEMA... SOMA HAPA...



 
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mpenzi wake Zarinah Hassan 'Zari'.

Kukubali! Baba mzazi wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa ‘Baba D’ amefunguka kuwa, kwenye listi ya wanawake wote waliowahi kuwa na mwanaye kimalovee, mwanadada Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ndiye mkwe wa ukweli kwake kutokana na kuwa tayari kumletea mjukuu.
Akizungumza  juzikati jijini Dar, baba Diamond alisema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo vilikuwa vikimkosesha amani ni maneno yaliyokuwa yakimsakama Diamond kuwa huenda hana uwezo wa kumpa mimba mwanamke, kiasi cha warembo wote aliowahi kuripotiwa kutoka nao kutoka patupu bila kushika ujauzito.
“Nawashangaa sana hao wanawake si huyo Wema (Sepetu) wala hao wenziye, maana Diamond alisema kampa mimba Penny (Penniel Mungilwa) zikatoka huku mwenyewe akikanusha hajawahi kushika mimba kwa kumchafua tu mwanangu aonekane siyo mwanaume rijali,” alisema mzazi huyo.

Baba mzazi wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa ‘Baba D’.
Baba D alitiririka kwamba mastaa hao wa kike ambao Mbongo Fleva huyo aliwahi kutoka nao huenda wao ndiyo hawana kizazi hivyo wanamtupia lawama mtoto wake kwa kushindwa kuwazalisha.
Alisema kuwa kikubwa anachokiamini wote hawakuwa na upendo wa kweli kwa mwanaye, walitaka kuzitumia tu fedha zake na kumuacha solemba lakini sasa Zari ndiye mwenye penzi la dhati kwa mwanaye.
“Kiukweli Zari kanifurahisha. Ndiye mkwe wangu wa kweli na halali kabisa.
“Nampongeza sana Zari kwa kushika ujauzito wa mwanangu. Sasa Diamond atatembea kifua mbele kwa kujiamini,” alisema baba D.
Alisema kutokana na kile kilichokuwa kikiaminika kuwa hana maelewano mazuri na mkali huyo wa Bongo Fleva, kwa sasa wapo vizuri na hata akiwa na tatizo huwa anamwambia Diamond ambaye amekuwa akimpa msaada.
“Kwa sasa nina maelewano mazuri na Diamond, muda wowote nikiwa na tatizo huwa namjulisha ananisaidia, kitu ambacho kinamfanya amgharamie mama yake kuliko mimi ni kwa sababu aliishi naye kwa kipindi kirefu na kuhangaika naye tangu utotoni,” alisema.
Ukiacha Zari ambaye amekubali kubeba ujauzito wake, Diamond aliwahi kuwalalamikia baadhi ya wapenzi wake kuwa walikataa kumzalia mtoto akiwemo Wema, Penny na Jokate Mwegelo.

Endelea kuperuz modesigntz, na mimi naendelea kukuwekea kila stori inayonifikia...

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU ILI NA WEWE UWE MWANACHAMA NA HABARI ZETU ZIKUFIKIE MOJA KWA MOJA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top