Akizungumza na gazeti hili baada ya kuombwa maoni yake, Kajala alielezea masikitiko yake juu ya hali ya rafiki yake wa zamani, lakini akasema anaamini hana tatizo kubwa la kumfanya asipate kabisa mtoto, isipokuwa anadhani bado hajampata mtaalamu sahihi wa masuala ya wanawake anayeweza kumsaidia tatizo alilonalo.
“Namuombea sana kwa Mungu, lakini sitaki kabisa kuamini kama hawezi kupata mtoto katika maisha yake, mbona bado kijana sana, atapata tu bwana,” alisema Kajala, ambaye ana mtoto aitwaye Paula.“Sitaki kuamini, roho inaniuma sana, namshauri Wema asiumie wala kuwa mnyonge. Na watu waache kumuumiza kwa maneno ya kebehi, lakini kama Wema akiwa tayari kulea mtoto wa mwenzake, anione, nina imani atapata mtoto atamlea na kumtunza kama wake.
Wengine waliompa pole na kumtakia nguvu kukabiliana na tatizo lake ni pamoja na Jini Kabula, Salome Urassa ‘Thea’, Aisha Bui, Amanda Posh na Baby Madaha ambaye alisema;
Endelea kufuatilia modesigntz Beste wangu, na mimi ntaendeleqa kukuwekea kila stori inayonifikia...
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU ILI NAWE UWE UKIPATA HABARI ZETU MOJA KWA MOJA.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN



Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.