Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

KINACHEENDELEA KENYA... WANAFUNZI WAENDELEA KUUAWA...SOMA HAPA...

Ke Attack

Hali bado sio shwari kwa wenzetu Kenya, jana taarifa kubwa iliyoripotiwa kwa siku nzima kutoka kwenye nchi hiyo ni ishu ya kuvamiwa kwa Chuo Kikuu cha Garissa, ambacho kiko karibu na mpaka wa nchi ya Somalia.

Wavamizi hao walivamia jana katika Chuo hicho na kuua walinzi wawili na baadae kuendelea kuwashambulia wanafunzi.

Idadi ya vifo iliyoripotiwa mpaka sasa ni watu 147, askari na Vikosi vya Jeshi la nchi hiyo wameendelea kuzunguka maeneo ya Chuo hicho.

Shambulio hili ni kubwa, linafananishwa na tukio la uvamizi wa Shopping Malls za Westgate, Nairobi September 2013 ambalo lilisababisha vifo vya watu 67 na wengine zaidi ya 170 kujeruhiwa.

Mpaka sasa wavamizi waliouawa ni wanne na mmoja wao amekamatwa.

.
Ramani ya Majengo ya Garissa University College.
Hii ni video iliyorekodiwa watu wakifanya jitihada za kukimbia mashambulizi hayo

Endelea kuperuzi modesigntz Beste wangu na mimi ntaendelea kukuwekea kila habari inayonifikia... 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU ILI HABARI ZETU ZIKUFIKIE MOJA KWA MOJA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top