Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na Siwema wakiwa na mtoto wao.Hivi karibuni, Nay na Siwema ambao walikuwa wapenzi kisha kumwagana, waligombana na kila mmoja kuzungumza lake juu ya mtoto wao huyo ambapo Siwema alidai si damu ya Nay wakati msanii huyo alisema ni damu yake.
Licha ya kupokea majibu hayo mazuri kwake, Nay aliyachukua majibu hayo kwa kuangua kilio cha furaha huku akieleza ya moyoni kuhusiana na sakata hilo.“Hili ni swala ambalo lilikuwa linaniumiza kichwa kila kukicha. Unajua kama mwanaume, mtu akwambie mtoto si wako unadhani ni maumivu kiasi gani utayapata? Inauma sana, mtu umelea kuanzia mimba hadi mtoto amezaliwa, si kitu kidogo.
Nay aliingia kwenye utata huo takriban mwezi mmoja uliopita baada ya kupishana kauli na Siwema ambaye alimfumania akiwa na mwanaume mwingine nyumbani kwake, jijini Mwanza na kuamua kumchukua mtoto kisha kuishi naye jijini Dar kwa msaada wa mama yake mzazi.
Endelea kuperuz modesigntz beste wangu, na mimi ntaendelea kukuwekea kiula inayonifikia...
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU ILI HABARI ZETU ZIKUFIKIE MOJA KWA MOJA ULIPO.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.