Mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Stop! Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ amemzuia mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The
Boss Lady’ kwenda kujifungulia nje ya Bongo pindi mambo yatakapokuwa
tayari.
Habari zilizonyakwa na Ijumaa Wikienda
kutoka kwenye chanzo cha ndani ya familia ya Diamond zilieleza kwamba,
tayari jamaa huyo amemuanzishia Zari kliniki Bongo.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.Akizungumzia ishu hiyo, Diamond alisema kuwa anatamani kuwa karibu na mama kijacho wake huyo hivyo ni kweli anataka mwanadada huyo ajifungulie Bongo.
Diamond au Baba Kijacho alisema lengo la kufanya hivyo ni ili iwe shangwe kwa familia nzima tofauti na atakapojifungulia nje ambapo familia italazimika kusafiri kwenda kumuona Chibu Junior.
Kwa mujibu wa Diamond, Zari ambaye ni mama wa watoto watatu akifukuzia huyo wa nne anatarajia kujifungua kati ya mwezi Julai au Agosti, mwaka huu.
Endelea kufuatilia modesigntz Beste wangu, na mimi ntaendelea kukuwekea kila stori inayotua kwangu
USISAHAU PIA KU LIKE PAGE YETU ILI HABARI ZETU ZIKUFIKIE MOJA KWA MOJA
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.