CHAMA
cha ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani kimeanza kuwapiga msasa viongozi wake
wa ngazi ya kata na vijiji kama sehemu ya kuwaandaa kabla ya uchaguzi
mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Mafunzo
hayo yameanza kutolewa juzi katika Wilaya ya Kibaha Mjini kwa
kuwahusisha wenyeviti, makatibu, watunza hazina, wajumbe wa vikao
mbalimbali na wanachama wengine.
Katibu
wa ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani, Mrisho Halphan, alisema lengo la kutoa
mafunzo hayo ni kutaka kila kiongozi atambue majukumu yake kulingana na
eneo analofanyia kazi ili kukifanya chama kiwe imara.
“Chama
chetu ni kipya, kwa hiyo, mafunzo hayo yatasaidia kuwapa washiriki
uelewa mpana juu ya masuala ya kisiasa kabla uchaguzi wenyewe haujafika.
“Lengo
letu tunataka kila kiongozi wetu aweze kutimiza majukumu yake bila
kumuingilia mwenzake, kwani wakati wa mafunzo washiriki wanapewa sera na
mikakati ya ACT katika kupambana na mafisadi,” alisema Halphan.
Pamoja
na mafunzo hayo kuanzia wilayani Kibaha Mjini, Halphan alisema
yatatolewa mkoa mzima wa Pwani kupitia Wilaya za Kisarawe, Bagamoyo,
Mafia, Mkuranga, Rufiji na Kibaha Vijijini.
Akizungumzia
uchaguzi mkuu, Halphan alisema chama chake kipo tayari kusimamisha
wagombea kila ngazi, ikiwemo urais, ubunge na udiwani, kwa kuwa
wamejipanga vizuri na wagombea wa nafasi hizo wanao.
Pia,
aliwataka wananchi wasisikilize propaganda za watu wanaotaka kukiharibu
chama hicho, kwa kuwa wanaamini kitakuja kuwa tishio kisiasa kwa siku
zijazo.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.