Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka watanzania kuipinga na
kutoikubali sheria ya mpya iliyopitishwa ya takwimu kwa madai kwamba
sheria hiyo inalenga kuzuia uhuru wa vyombo vya habari na kuwanyima
watanzania haki na uhuru wa kupata habari.
Akihutubia
hivi karibuni mjini Bukoba katibu mkuu wa chama cha demokrasia na
maendeleo Chadema Dk. Wilibroad Slaa alisema kupitishwa kwa sheria hiyo
kunalenga kunyima uhuru wa habari pamoja na kuwafanya watanzania
kuendelea kubaki gizani na kuishi kama wapo shimoni bila kuelewa maovu
yanayofanywa na viongozi wasio waadilifu wanaotumia madaraka vibaya kwa
masalahi yao binafsi.
Alisisitiza
kuwa nia ya serikali kutaka kuzuia uhuru wa vyombo vya habari ni
kuwarudisha nyuma watanzania ili waweze kuishi bila kupata habari kama
ilivyokuwa enzi za ukoloni na kwamba hali hiyo haiwezi kuvumiliwa kwani
serikali inataka kuficha maovu ambayo yanaweza kuliangamiza taifa hapo
baadae.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.