Moja ya Habari kubwa kwenye siasa za Tanzania
katika kipindi cha wiki iliyopita ilikuwa habari ya CCM kuwafungulia makada wake sita ambao
walikiuka kanuni za chama hicho kwa kutangaza kugombea Urais mapema
kinyume na utaratibu wa chama hicho, mmoja wa Makada waliokuwa wamefungiwa ni
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mh.Edward Ngoyai Lowassa.
Jana kulikuwa na Habari ya Naibu Waziri Mwigulu Nchemba kutangaza kugombea Urais wa Tanzania kupitia CCM.. leo Mbunge Edward Lowassa
ameongea kuhusu mambo kadhaa ikiwemo hali ya afya yake, chuki ndani ya
chama, na ujumbe wake kwa CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 TZ.
Ishu ya chuki kwenye siasa >>”Kuna
chuki imeibuka kwenye siasa za nchi yetu na kutakiana mabaya, afya ni
neema kutoka kwa Mungu.. mimi niko sawa kabisa kwa chochote kile..
kwenye Chama chetu waweke utaratibu tukapimwe wote afya mimi nitakuwa wa
kwanza kwenda kupima tuelezane nani mgonjwa“>> Edward Lowassa.Sentensi yake nyingine kuhusu tatizo la ajira>>>”Tatizo la ajira ni bomu lisiposhughulikiwa.. toka nimetoka Serikalini kuna vitu ambavyo kama tungevifanya kwa kasi ile ambayo tulianza nayo ningepita napunga mkono nikapata kura zote, hatufanyi maamuzi iwe magumu au rahisi.. mambo yanakwenda legelege, Rais amefanya jitihada kubwa sana lakini kuna mambo hayaendi>>> Edward Lowassa.
Suala la elimu>>>”Tukiwekeza vizuri katika elimu tunaweza kubadilisha nchi yetu.. Tukitaka kuokoa nchi yetu tuwekeze kwenye elimu“>>> Edward Lowassa.
Kuhama CCM je? >>>”Kuhama chama sina mpango.. nimeingia CCM toka 1977 sijafanya kazi mahali pengine popote isipokuwa CCM.. My life is CCM.. huyo ambae hanitaki CCM ndio ahame sio mimi nihame“
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.