ILIPOISHIA
SEHEMU YA 24
... Mzee Bisu
alisogea mlangoni akachungulia hakuona mtu pale sebuleni hakuona mtu, akatoka
haraka na nakuongoza kwenye korido ya kuingilia chumbani kwake, lakini kabla
hajafika akakutana uso kwa uso na mwanaye Dennis ambaye naye alikuwa akitokea
chumbani kwake...
SASA ENDELEA
NA SEHEMU YA 25
... Mzee Bisu
alipatwa na mshituko mkubwa ambao kama mwanaye angekuwa makini kumtizama
angeweza kumgundua.
“... Shkamoo
baba...” aliamkia Dennis akiwa kasimama palepale mbele ya mlango wa chumba
chake.
“... Marhaba
Dennis, kumbe ulisharudi?..” alijibu na kutupia swali moja kwa moja huku
akijitahidi ili mwanaye huyo asiweze kugundua kitu, na baada na kuuliza swali
hakusubiri jibu aliendelea kutembea kuelekea mlango wa chumbani kwake, alifanya
hivyo kwa kuhofia mwanaye asiweze kugundua chochote kwani toka amalize kurusha
roho na msichana wa kazi alikuwa hata hajajimwagia maji.
“... mimi
nilisharudi muda alafu nikaona gari lako limepaki hapo nje lakini nikawa siuoni
humu ndani, nilijaribu kugonga mpaka mlango wako lakini haukuwepo...” aliongea
kwa kirefu Dennis kujari kujuwa ni wapi alikokuwa baba yake, lakini baba yake
hakujibu swali hilo kwani mpaka Dennis anamaliza kuongea Mzee Bisu alikuwa
tayari alishazama chumbani kwake. hata hivyo hakupenda kufuatilia sana kwani
hakumuhisia kitu chochote na wala alikosa uhusiano wa uwepo wa baba yake pale
nyumbani na tukio lake na msichana wa kazi Hasina.
*******************
Mzee Bisu
alinogewa sana na penzi la msichana huyo wa kazi akajikuta amezama kabisa
mapenzini akaanzisha tabia ya kukutana na hasina nje ya pale nyumbani yaani
kwenye nyumba za kulala wageni. kwa upande wa hasina naye alibadilika kutoka
katika hali ya ule ushamba ushamba na kuwa msichana wa kisasa kabisa kuanzia
mavazi mpaka muonekano, akaanza pia tabia ya kuchelea kila anapokwenda sokoni
na wakati mwingine akiulizwa anajibu mkato tofauti na zamani alivyokuwa na heshima
za kijijini. lakini pia kwa upande wa Dennis moyo ulizidi kudidimia na kujikuta
naye akimtaka Hasina kwa hali na mali lakini kila akijaribu kuwa naye karibu
Hasina alikuwa akimkwepa kitu ambacho mara nyingi kilikuwa kinampa hisia za
kuwa Hasina ana mwanamme, akaanza kufanya uchunguzi ili aweze kumbaini huyo
mwanamme.
Mabadiliko
hayo ya Hasina pia yalimtia wasiwasi mke Bi. Pauline, na kuanza kujiuliza
maswali kibao kutokana na mabadiliko ya ghafla ya msichana wake wa kazi akajiapiza
kumchunguza taratibu, hakupenda kumuonesha kuwa alishashitukia mabadiliko yake
na wala hakupenda kuongelea kitu kulingana na kuchelewa kwake kila anapotumwa
sokoni au majibu yake ya mkato na jeuri ndani yake. Bi Pauline alijaribu siku
moja kuliongelea hilo kwa mume wake lakini mume wake alimtetea Hasina.
“... muacheni
motto wa watu naye aishi kama wasichana wengine jamani, mbona mnamsakama?..”
hayo ndio yalikuwa majibu ya Mzee Bisu
“... lakini
Baba Dennis, huyu mtoto wa watu na tulikabidhiwa sisi pamoja na kuwa
anatusaidia kazi, na pale anapopotoka tunatakiwa kumnyoosha kwa ni kama mtoto
wetu pia...” alijibu Bi. Pauline.
“...
umnyooshe kwani amefanya nini?.. aulishamkuta na mwanaume?..”
“... ina
maana Baba Dennis we huoni mwenendo wa mtoto huyu kuwa umebadilika?..”
“... muache
mtoto naye aishi kwa amani... msimnyanyase... akishajibu hivyo huondoka kabisa
karibu na mkewe.
*************
Ilikuwa siku
ya Jumamosi, siku ambayo familia nzima ya Mzee bisu hushinda nyumbani ukiachia
wale watoto wake wa kubwa wanaoishi nje ya nchi, siku hiyo kila mtu anakuwepo
maeneo ya nyumbani na kila mtu anakuwa busy na mambo yake lakini inapofika muda
wa chakula wote hukusanyika na kula chakula pamoja katika meza moja.
lakini siku
hiyo ni siku pia ambayo Mzee bisu aliipania ili apate kula tundi na Hasina,
lakini kila alipokuwa akitafuta chance ya kumtoa pale nyumbani wakatafute
sehemu wabanjuke, hali ilikuwa imebana sana kwani Bi. Pauline naye alikuwa
kaaribusana na hasina akimtumia katika shughuli za hapa na pale, na ilipofikia
swala lakwenda sokoni ambapo alitegemea itakuwa chansi nzuri, Bi. Pauline
alibana nay eye ndio akaamua kwenda sokoni siku hiyo.
hiyo pia
ilikuwa chansi nyingine, lakini ikawa ngumu kwani nyumbani hapo alikuwepo
mwanaye Dennis ambaye naye kwa udi na uvumba aikuwa alitafuta nafasi nzuri ya
kuwa na Hasina siku hiyo. sasa ikawa kuviziana Hasina akiingia chumbani kwake,
Mzee Bisu anazengea maeneo hayo kutafuta nafasiya kuzama chumbani kwa Hasina.
lakini nafasi ikawa haipatikani kwa
Dennis naye anakuwa amesogea sebuleni kutafuta nafasi ya kuomba mechi
siku hiyo, hivyo wote wanajikuta wakiwa sebuleni na kubaki wakiangaliana na mtu
asiwezekuongea chochote kwa mwenzake.
Hasina
anapotoka chumbani kuingia jikoni, Dennis anaakti kuchukua galsi nakwenda
jikoni kwa nia ya kuchukua majikwenye jokofu ambapo nafasi hiyo aitumie
kumpanga Hasina, ni kama Mzee Bisu naye alikuwa akihisi kitu, naye anainuka
nakuingia jikoni na kujifanya kuna kitu anakihitaji kwa Hasina hivyo kila mmoja
akakosa nafasi ya kupata kile alichokihitaji.
lakini mzee
Bisu akapata mbinu, wakiwa wamekaa wote pale sebuleni wakiviziana, Mzee Bisu
akamuita Hasina, alipofika akamwambia.
“... pale juu
ya kabati chumbani kwangu nafikiri kuna kitabu changu kile nilikuwa nasoma jana,
kakichukuwe uniletee...” aliongea mzee bisu huku akiwa kamtolea macho Hasina.
bila kuongea
neno Hasina aliingia chumbani kwa mzee bisu kwenda kuchukua hichokitabu, lakini
ukweli nikwamba hichokitabu hakikuwepo, alifanya hivyo ili Hasina achukuwe muda
kukitafuta ili nay eye amfuate hukohuko. na ndivyo ilivyo tokea, baadaya kuona
Hasina anachelewa, Mzee Bisu alinyanyuka na kumfuata Hasina chumbani Kisha
mlango ukajirudisha.
lakini
kitendo hicho nikama kilimyima Dennis amani na kuanza kumfikiria baba yake
vibaya kuwa labda naye atakuwa analitafuta tundi la Hasina, akatamani kuinuka
aende mlangoni kwa baba yake akachungulie au kusikiliza nini wanachokiongea
chumbani humo. alipokuwa akitaka kunyanyuka alisikia gari likipaki nje ya
nyumba yao akasita kusimama pale alipokaa mara mlango wa mbele wa nyumba yao
ukafunguka na mama yake Bi. Pauline akaingia akiwa amebeba mfuko yenye bidha tofautitofauti
aliyotoka nayo sokoni... Dennis alishituka na kuingiwa na uoga kuwa mama yake
anaweza akamkuta baba yake na Msichana wa kazi chumbani kwao akawa anamuangalia
mama yake kasha anaangalia mlangoni katikachumba cha wazazi wake kama
watatokea....
NINI
KITAENDELEA... USIKOSE SEHEMU YA 26
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.