Mwigulu Nchemba.
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba amejiuzulu nafasi hiyo ili awanie
nafasi ya kugombea urais na nafasi yake imechukuliwa na Rajab Luhavi
aliyekuwa mshauri wa rais katika siasa.
Mwigulu amabye pia ni Naibu Waziri wa
Fedha, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo naja jioni katika Kikao cha
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mkoani Dodoma.
Akithibitisha taarifa hiyo, Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kuwa Mwigulu ameamua
kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na nia yake ya kutaka kuomba kuwania
urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka
huu.
"Mwigulu alikuwa ameshamwambia nia hiyo
Mwenyekiti wa Chama, Rais Jakaya Kikwete, naye akamkubalia, sasa leo
katika kikao ameomba rasmi kujiuzulu na mwenyekiti amemkubalia mbele ya
wajumbe wa NEC" Alisema Nape.
Nape amesema kufuatia uamuzi huo,
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete amemteua msaidizi wake katika masuala ya
siasa, Ndugu Rajabu Ruhavi kuwa Mjumbe wa NEC, na wakati huohuo kumteua
kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM kushika nafasi iliyoachwa na Mwigulu.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.