Ni
nadra sana kukutana na Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi maarufu kama K-Lynn
lakini kupitia tuzo za watu tulifanikiwa kupiga story mbili tatu.
K-Lynn amefunguka kuwa maisha akiwa kama mama watoto wawili mapacha yamekuwa ya aina yake na anayafurahia kila sekunde.
“Nimejifunza
kuwa mvumilivu, nimejifunza upendo ambao sijawahi kujisikia kabla.
Jinsi unavyompenda mtoto ni tofauti ambavyo unaweza kumpenda mtu yoyote
yule katika maisha yako,” alisema.
Katika hatua nyingine Miss Tanzania huyo wa zamani alisema hakuna uwezekano wowote wa yeye kurejea tena kwenye muziki.
“Kwa
bahati nzuri sana baada ya kufanya uamuzi wa kutokuwa kwenye muziki,
niliweza kupata kitu kingine ambacho kimeuteka moyo wangu. Kufanya
interior design kunanifurahisha kuliko hata muziki.
"Nafurahi
sana kujua kwamba kuna watu wangependa kunisikia ama kusikia nikiimba
lakini nafikiri moyo wangu umehamia kwenye sanaa nyingine.”
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.