Mshangao huo wa wadau wa RAPEE, ulikuja baada ya video yake mpya kukamilika na kusambazwa kwenye mitandao, ambapo watu wengi walijitokeza na kusema kuwa huyu ndio alitakiwa kupambana na Diamond kimuziki na sio Ali Kiba kwani anauwezo mzuri wa kuimba na kisha anauwezo wakucheza na Camera anapokuwa anafanya Video.
"... huyu dogo ni shida,.. huyu ndo saiz ya Platnumz sasa sio kina Kiba..."
alicomment mdau mmoja katika post za mtandao wa intagram.
Kama hiyo haitoshi, wengi wao waliipongea video kwa ubora wake na kusema haina tofauti na hizo zinazotoka South Africa. pia wakasema kuwa RAPEE akipata sapoti nzuri anaweza kufika mbali kama wanamziki wengine.
Rapee alishawahi kutoa nyimbo nyingine ambazo zilijitahidi kufanya vizuri siku za nyuma japo hazikumfikisha alipokusudia kufika zilizokuwa zikijulikana kwa majina ya Umeme UmerudiI, Remix ya Mery me ya Rich Mavoko na Mashetani.
Ngoma hii ya Natamani ilitengenezwa na Producer wake mkongwe Promise Nyota na Video ikafanywa na kampuni ya EXPERIENCE PICURE chini ya Director Bancell Otieno.
Kwa sasa Rapee bado hana Management, anapewa support na makapuni Machanga yaliyoko katika muunganiko wa SUPPORT MUSIC AFRICA kama vile,
FIRE MUSIC, EXPERIENCE PICTURE, STREET EYE MEDIA, PROUD AFRICA NA MO DESIGN
BOFYA HAPA KUONA VIDEO
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.