MBUNGE
wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) jana nusura apigane na
askari aliyekuwa akilinda kituo cha kujiandikisha katika daftari la
wapiga kura cha Shule ya Msingi Mkombozi Kata ya Sokoni I.
Tafrani hiyo ilitokea saa 5.00 asubuhi wakati Mbunge huyo
alipokuwa
akitembelea vituo vya kujiandikisha kupiga kura jijini Arusha
akifuatana na waandishi wa habari. Uandikishaji huo ulianza juzi.
Lema
alipofika kituoni hapo alikuta foleni kubwa nje ya lango la kuingia
kituoni hapo huku ndani ya lango hilo akiwamo askari wa kike aliyekuwa
amevalia kiraia.
Askari huo alikuwa akiandikisha majina ya wananchi hao na kuwataka waondoke hadi kesho yake kupata vitambulisho.
Kutokana
na hali hiyo Lema alibishana na askari huyo ambaye jina lake halikuweza
kupatikana na kumnyang’anya kalamu aliyokuwa akitumia kuandika majina
hayo katika daftari dogo huku akiwaambia polisi hao wanavunja sheria.
Majibizano
kati ya Lema na askari huyo wa kike yalisababisha askari mwingine wa
kiume kuingilia kati na baada ya mabishano makali na Lema, walishikana
wakitaka kupigana kabla ya kuamriwa na viongozi waliokuwa wamefuatana
na Lema.
“Haiwezekani polisi akaandikisha majina na kuwaambia watu waje siku inayofuata waweze kufanya taratibu za kupewa vitambulisho.
”Polisi
wajibu wako hapa kituoni ni kuangalia usalama na siyo vinginevyo,
utaratibu mnaoufanya ni kosa. Hata mawakala wa vyama vya siasa waliopo
hapa hawana majina haya.
“Tutajuaje
mnaenda kuyabadilisha au kuuza hili daftari na kutuletea majina mengine
... na daftari hili halina muhuri wa aina yoyote,”alisema Lema.
Tafrani
hiyo ilisababisha Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha (OCS),Thomas
Mareko kufika kituoni hapo naye akaendelea kubishana na Lema
aliyesisitza kuwa polisi walikuwa wanafanya makosa.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.