
Kama wewe ni mtu wa fashion na style za
kisasa kwenye ishu ya mavazi, basi hii stori iwe karibu na wewe…
fasion za mtu kuvaa nguo za kubana hua zipo tu siku zote, lakini umeipata stori ya
Australia kilichomkuta mtu aliyevaa suruali yakubana?..
Ripoti kutoka Australia inahusu ishu ya
mwanamke mmoja kulazwa Hospitali kwa muda wa kama siku nne hivi, kutokana na
mishipa yake kupata majeraha baada ya kuvaa nguo ya kubana alafu
akachuchumaa kwa muda mrefu.
Mwanamke huyo alijisikia kama ganzi
hivi alipoinuka, akajaribu kutembea lakini hakufika mbali.. alianguka na
baada ya muda kidogo alipata msaada wa kufikishwa Hospitali.
Dr. Thomas Kimber ni daktari katika Hospitali ya Royal Adelaide,
Australia ambapo mwanamke huyo alipelekwa kutibiwa… Dokta anasema
alishangazwa na jinsi ambavyo mgonjwa huyo alipata majeraha hayo
yaliyotokana na nguo aliyoivaa.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.