Mwandishi wetu
NGOMA
nzito inaripotiwa kuwepo baina ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kada wake
mkongwe, Edward Lowassa ambaye hivi karibuni alihamia Chadema, baada ya
pande hizo mbili kutupiana shutuma, kila mmoja akimponda mwenzake.
Wakati Waziri Mkuu wa zamani Lowassa,
ambaye Jumanne iliyopita alitangaza rasmi kuhamia Chadema akisema
mchakato wa kumtafuta mgombea urais wa CCM ulijaa chuki na mizengwe
dhidi yake, wenzake wamemuita kama mtu mwenye tamaa ya madaraka,
asiyepaswa kuaminiwa.
Kuonesha kuwa pande hizo mbili hali ni
tete, juzi CCM ilishindwa kuzungumzia suala hilo la kuhama kwake katika
mkutano ilioitisha na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, badala
yake ikatumia nafasi hiyo kuwashukuru wanahabari na wakazi wa jiji hilo
kwa mapokezi mazuri kwa mgombea wao wa nafasi ya urais, Dk. John Pombe
Magufuli.
Wajumbe wa Kamati Kuu CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wao Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Vigogo wa CCM, akiwemo Katibu wa Itikadi
na Uenezi Nape Nnauye ambaye analaumiwa kuongoza harakati za
kumshambulia Lowassa kabla ya mchakato huo, wamekataa kuzungumzia kuhama
kwa kada huyo, lakini katika mitandao mbalimbali ya kijamii, upo
mvutano mkubwa miongoni mwa wafuasi wa pande hizo mbili.
Lowassa akionesha fomu ya kugombea urais.
Wakati wafuasi wa CCM wakikebehi hatua
hiyo na kumwelezea kama mtu anayeweweseka, mroho wa madaraka na fisadi
asiyefaa kupewa nchi, Team Lowassa wanawaelezea wapinzani wao kama wenye
wasiwasi wa kushindwa, kutokana na mtu wao kuwa kipenzi cha watu wengi
nchini.
Lowassa, alikabidhiwa kadi ya uanachama
wa Chadema yeye na mke wake, Regina Jumanne wiki hii, akirejea kauli ya
Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kuwa chama hicho tawala siyo mama
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.