Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Na Makongoro Oging’
WANACHAMA wa
kundi la Marafiki wa Edward Lowassa waliochanga fedha za kumwezesha
waziri mkuu huyo wa zamani kuchukua fomu ya kugombea urais, wamemtuhumu
aliyekuwa naibu katibu wao, George Kivuyo (pichani) kutafuna fedha
hizo.
Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi
ya wanachama hao wanaojulikana kama Team Lowassa 4 President, zinadai
naibu katibu mkuu huyo ambaye pia ni mweka hazina wao, alitafuna kiasi
cha shilingi laki saba zilizochangwa.
Walidai fedha hizo ziligunduliwa
kutotumika ilivyopaswa baada ya kutojulikana zilipo na alipoulizwa
hakuwa na majibu ya kueleweka.
Baadhi ya wanachama hao, Fauzia Ally,
Hassan Mollel na Yussuf Hamis walisema kutokana na kitendo hicho,
wanachama hao wameanza kufarakana kutokana na mgogoro.
“Hizi fedha zilitumiwa tofauti na ilivyokusudiwa, zinatakiwa zirudishwe, akabidhiwe mzee Lowassa,” alisema Hassan Mollel.
Naibu katibu mkuu huyo alipopigiwa simu
na mwandishi wetu juzi Jumapili alisema kwamba madai hayo ni ya uongo na
fedha hizo hazikuwa laki saba bali zilikuwa Sh. 526,000.
“Mimi ni mweka hazina msaidizi na tatizo limekuja baada ya kuhoji kuhusu fedha hizo alizokabidhiwa bosi wangu.”
Katibu mkuu wa chama hicho, Mohamed
Mkindi alipoulizwa alikiri kusikia malalamiko hayo lakini alidai yupo
mikoani na akirudi jijini Dar es Salaam atazifuatilia.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.