SIMULIZI inashangaza! Hussein Mohamed (28) amewekewa msiba nyumbani kwa wazazi wake baada ya kuambiwa kijana huyo amefariki dunia.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni Magomeni ya Makuti, Dar ambapo habari zilisema, Hussein alicharangwa mapanga Vingunguti Dar na watu wasiojulikana na amefariki dunia.
Wakizungumza na wakati watu wakiondoka ‘msibani’ hapo, baadhi ya majirani walisema wanandugu walishasambaza habari mikoani kwa ndugu lakini ghafla, walisikia marehemu ameonekana duka la jirani akinunua sigara.
“Yaani wengine tulishaanza kupanga mazishi yawe wapi. Tulivyosikia marehemu kaonekana, watu walikimbia hovyo. Sisi majasiri tukamfuata dukani kumuuliza kulikoni, mwenyewe akashangaa,” alisema moja wa majirani.
Naye Hussein mwenyewe akizungumza na gazeti hili alisema:
“Siku ya tukio nilikuwa nakunywa pombe na marafiki zangu, Manzese (Dar). Nikaibiwa simu. Huyo aliyeniiba ndiye aliyepiga simu nyumbani kuwaambia nimeuawa kwa kucharangwa mapanga.
“Nimeshangaa sana kukuta watu wananizunguka wakisema nimefufuka. Mimi nipo hai na nina afya yangu kama kawaida.”
tulilizungumza na mama yake Hussein, Amina Chomela (55) aliyesema siku ya tukio alipokea simu kwa namba ya Hussein na kuambiwa mwanaye huyo alicharangwa mapanga na kufa maeneo ya Vingunguti.
“Niliangua kilio, majirani walikuja kuanza kuomboleza. Lakini nimefurahi mwanangu amerudi akiwa hai,” alisema Amina.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.