KARIBU msomaji wangu katika ukurasa huu ambao tumekuwa tukifundishana mengi yahusuyo afya zetu na tukipeana elimu ya kuboresha afya zetu.
Wiki iliyopita tuliangalia tatizo la mwanamke kukosa hedhi na tukazipitia baadhi ya sababu au vyanzo vya mwanamke kukosa hedhi. Napenda kukukumbusha kuwa mwanamke kukosa siku zake au hedhi kumegawanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni wale wanaokosa siku zao kwa kawaida bila ugonjwa na kundi la pili ni wale wanaokosa siku zao kwa sababu ya ugonjwa.
Tulianza na vyanzo au sababu ambazo si za ugonjwa zinazoweza kumfanya mwanamke asipate hedhi na moja kubwa ni tabia ya maisha yake ya kila siku, yaani vyakula anavyokula (life style).
Sababu nyingine zinazosababisha mwanamke kukosa hedhi ni kama zifuatazo:-

Matatizo katika mfumo wa homoni
Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa katika tezi za hypothalamus, pituitary au ovary.
Matatizo katika Hypothalamus: Matatizo katika hypothalamus yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi ni pamoja na uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitary.

Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi.
Matatizo katika tezi ya Pituitary: Vyanzo vinavyohusisha tezi ya pituitary ni pamoja na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu au kwa kitaalamu Prolactinemia. Prolactin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha.

Hali ya kuwa na prolactin nyingi katika damu inaweza kutokea iwapo kuna uvimbe unaoitwa (prolactinoma) katika tezi ya pituitary. Kuwepo kwa uvimbe mwingine wowote katika tezi ya pituitary.
Ikiwa pituitary itashindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa, hususan iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua. Hali hii husababisha kuharibika kwa tezi ya pituitary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili.

Hali hii husababisha kuwa na mfumo mbovu katika afya ya uzazi na kusababisha mwananmke kukosa hedhi.
Matatizo katika ovary: Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike yaani ovaries ni pamoja na kutozalishwa kabisa kwa mayai (Anovulation)

Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu (Hyperandrogenemia) Ovary kuwa na vifukovifuko (polycystic ovarian syndrome) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri.
Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa.
Vilevile kuna tatizo la kufa na kushindwa kufanya kazi kwa ovary kabla ya muda wake pamoja na ugonjwa wa kuzaliwa unaoitwa Turner Syndrome ambao huambatana na kukosekana kwa ovary au ovary kuwa changa kuliko kawaida, msichana kushindwa kuvunja ungo na msichana kuwa na kimo kifupi kuliko kawaida.
Ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kijenitikia (genetic disease).
Matatizo katika ovary yanasababishwa na:

Ukosefu wa kimaumbile wa ovary ambao hutokea wakati wa ukuaji.
Kufa kwa ovary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili.
Historia ya kuwahi kupata tiba ya mionzi au madawa yanaathiri ovary.
Ugonjwa wa kurithi wa Galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango cha juu cha sukari aina ya galactose katika damu.

Habari njema ni kwamba pamoja na matatizo haya kuwasumbua wanawake wengi kuna mimea tiba ambayo inaweza kuondoa matatizo haya. Ili ujue tatizo lako ni vema ukawaona madaktari kwa uchunguzi.
Pia unaweza ukatembelea Sigwa Herbal Clinic kwa uchunguzi na matibabu ya uhakika.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.