…Akisaini katika kitabu cha wageni kwnye moja ya ofisi za CCM mikoani.
TAYARI Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kimemtangaza Waziri wa Ujenzi, John Pombe Joseph
Magufuli kuwa mgombea urais mwaka huu huku Samia Suluhu Hassan akiwa
mgombea mwenza, lakini bado jina la mgombea aliyekatwa, Edward Lowassa
linazungumzika, safari hii yakibainishwa mambo matano yanayoolezwa ndiyo
yalichangia kukatwa kwake.
Akizungumza na Uwazi juzi mjini hapa kwa
sharti la kutotajwa jina lake gazetini, mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu
ya CCM-Taifa (Nec) alisema nguvu ya Lowasaa kichama ilikuwa kubwa
lakini mambo hayo matano ndiyo yalisababisha akashindwa kufikia hata
hatua ya Tano Bora.
“Sisi kama wajumbe, tunajua mengi.
Lowassa alikuwa mgombea mwenye nguvu, alikuwa na watu ndani ya Nec,
lakini sasa Kamati Kuu (CC) ilimkata kwa vigezo vyake, lakini naamini
ndani ya hayo mambo matano ndiyo maana alikatwa.
MAKANISA, MISIKITI YATAJWA
Kwa mujibu wa mjumbe huyo kutoka Mkoa wa Tanga, kitendo cha Lowassa kuchagisha fedha kwa njia ya harambee kwenye misikiti na makanisa akiwa kama mgeni mwalikwa, kulichangia CC ya CCM kumwona kama alianza kampeni mapema.

“Unajua ndani ya makanisa mengi
yanasemwa. Baadhi ya watu ndani ya chama chake walisema alianza kampeni
mapema kwa vile kule kuzungumza na waumini kuliweza kumpa nguvu ya
kisiasa. Hii nayo ilichangia,” alisema mjumbe huyo.
…Akikusanya fomu za zilizosainiwa na wadhamini.
STAILI YA KUTANGAZA NIA
Mjumbe huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, jambo la pili ambalo lilimtia doa ya kuteuliwa Lowassa ni staili aliyoitumia kutangaza nia.
Mjumbe huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, jambo la pili ambalo lilimtia doa ya kuteuliwa Lowassa ni staili aliyoitumia kutangaza nia.
Alisema: “Unajua CCM inakataza kabisa
mtu mwenye kutangaza nia kufanya vitendo vyovyote vyenye dalili ya
kampeni. Lowassa alipoyakaribisha yale makundi ya kumshawishi kugombea
na kuzungumza na vyombo vya habari pia ilikuwa ni kigingi kwake. Kama
itakumbukwa kuwa, kuna wakati Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
ilibidi aseme.”
KUFUNGIWA NA KAMATI
“Pia itakumbukwa kuwa, Februari 18, mwaka jana, Kamati Kuu ya CCM iliwafungia makada wake sita kwa kosa la kuanza kampeni mapema jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa chama.
“Pia itakumbukwa kuwa, Februari 18, mwaka jana, Kamati Kuu ya CCM iliwafungia makada wake sita kwa kosa la kuanza kampeni mapema jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa chama.
“Lowassa alikuwemo, lakini wengine pia
walikuwemo kama Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa), Januari Makamba (Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia), William Ngeleja (Mbunge wa Sengerema), na Frederick Sumaye
(waziri mkuu msatafu).
“Sasa, walipofunguliwa, Lowassa
alionekana kama anaendelea kwa kitendo chake cha kuzungumza na wananchi
kwa kupitia kigezo cha makundi kwenda kumshawishi,” alisema mjumbe huyo.
MATAJIRI, WAFANYABIASHARA WAKUBWA
Kitendo cha kudaiwa kuwa na ukaribu na baadhi ya matajiri na wafanyabiashara wakubwa ambao wanatiliwa shaka na baadhi ya wananchi pia kunatajwa kuwa sababu ya CC kuamua kumuweka kando Lowassa.
Kitendo cha kudaiwa kuwa na ukaribu na baadhi ya matajiri na wafanyabiashara wakubwa ambao wanatiliwa shaka na baadhi ya wananchi pia kunatajwa kuwa sababu ya CC kuamua kumuweka kando Lowassa.
DOA LA RICHMOND
Licha ya mwenyewe kuwahi kusema mbele ya mkutano mkuu wa Nec wakati fulani kwamba, katika mchakato wa upatikanaji wa tenda ya kufua umeme kwa Kampuni ya Richmond, hakuna alilolifanya bila serikali kuu kujua lakini bado doa lile lililosababisha akajiuzulu uwaziri mkuu limeonekana kuwa kikwazo kwake.

“Ni kweli Lowassa alijiuzulu kwa sababu
ya nafasi yake lakini si kwamba alihusika na ufisadi. Lakini nahisi iko
haja kwake kuweka bayana kuhusu ule mchakato kwani baadhi ya wanasiasa
wenzake wamekuwa wakitumia ishu ile kama jiwe la kumpigia.
“CC iliona kwamba, kama wangempeleka
yeye kwenye kinyang’anyiro labda wapinzani wangetumia sakata la Richmond
kujizolea kura kwa madai kwamba, Lowassa alijiuzulu kwa sababu hiyo,”
alisema mjumbe huyo.
KUTOKA NDANI ZAIDI
Hata hivyo, pia kuna madai kwamba, wajumbe wa CC walimtafakari Lowassa kwa umakini na kugundua kuwa, alitakiwa kukatwa jina mapema kabla ya kuingia kwenye Tabo Bora.
Hata hivyo, pia kuna madai kwamba, wajumbe wa CC walimtafakari Lowassa kwa umakini na kugundua kuwa, alitakiwa kukatwa jina mapema kabla ya kuingia kwenye Tabo Bora.
“Kama Kamati Kuu ya CCM ingempitisha
Lowassa kwenye Tano Bora, hakuna ambaye angemshinda mbele ya safari
kwenye Nec na Mkutano Mkuu. Alikuwa na nguvu kubwa kwa wajumbe. Ndiyo
maana wakamdhibiti kule mwanzoni kabisa,” kilisema chanzo kimoja na
kuongeza:
“Lakini hata Nec na Mkutano Mkuu
walipopelekewa jina la Magufuli walifurahia kwa sababu hana makundi
ndiyo maana akazoa hizi kura 2104 na ndiye mgombea aliyepeleka hofu
kwenye vyama vya upinzani (Ukawa) kwa sababu hana kashfa.”
KISA CHA KUKATWA MEMBE
Chanzo hicho kilisema kuwa, Bernard Membe ilibidi akatwe ili kutuliza upepo wa kisiasa ndani ya chama.
“Unajua Membe ndiye aliyekuwa mpinzani mkubwa wa Lowassa. Kuingia kwake kwenye Tano Bora na kuachwa Lowassa kusema kweli kulizua taharuki kubwa. Baadhi ya watu walikusudia kuibua uasi. Ndiyo maana ukawasikia wajumbe wakiimba wana imani na Lowassa wakati mwenyekiti wetu (Jakaya Kikwete) akiingia ukumbini.

“Ilibidi jina la Membe likatwe ili kambi
ya Lowassa waone kifo cha wengi ni harusi na upepo mbaya ukatulia ndani
ya chama la sivyo mpaka leo (Jumapili) kungekuwa bado Tano Bora iko
mikononi mwa wajumbe wa Nec,” kilisema chanzo hicho.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.