Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

WOLPER: MIMI NA LOWASSA HADI KIFO... SOMA KWA NINI?..

jackline-wolper1Staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper.

STAA wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita kufuatia kambi yake ya kisiasa ya Edward LowassaTimu Lowassa’ kukatwa jina kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka huu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku akisema yeye na Lowassa ni mpaka kifo
_MG_4379_1Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja ambacho ni rafiki wa Wolper (jina lipo), Jumamosi usiku aliposikia kwamba, jina la Lowassa lilimegwa kwenye mchakato wa Kamati Kuu ya CCM (CC), staa huyo alianza kulia huku akisema amekwisha!
“Sijui Wolper aliahidiwa nini? Amelia sana kukatwa kwa jina la Lowassa. Wakati akilia alikuwa akisema amekwisha. Sasa sijui alikwisha nini?” kilisema chanzo hicho.
Wolper alipotafutwa na gazeti hili kwa lengo la kuthibitisha madai hayo, alikiri kumwaga machozi kwa sababu ya ushabiki wake wa kisiasa.
“Nililia sana, sana, sana tena sana kwa sababu nilijipa matumaini kuwa yeye atashinda. Hata hivyo, mimi ni Lowassa tu mpaka kufa. Mimi sina chama wala sina kadi lakini nampenda tu Lowassa. Ni mchapa kazi,” alisema Wolper.
Akaongeza: “Ila sijakata tamaa, Lowassa ndiyo rais wangu kivuli. Nitakuwa namuita mheshimiwa rais.”
Kuhusu kudai amekwisha, Wolper alisema: “Sikuahidiwa chochote, bali kuna waigizaji wenzangu tulipingiana. Sasa kushindwa kwa kambi yangu si lazima niseme nimekwisha jamani!”
Katika kinyang’anyiro hicho, Lowassa alikuwa akichuana na wagombea wengine 38 wa chama hicho, lakini jina lake lilikatwa katika hatua za awali na kuwaacha kwenye Tano Bora, January Yusuf Makamba, Balozi Amina Salum Ally, Asha–Rose Mtengeti Migiro na John Pombe Magufuli ambaye aliibuka kidedea

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top