Baada ya kuwa kuna kila dalili ya uhamisho wa Pedro Rodriguez kujiunga na klabu yaManchester United kukamilika akitokea FC Barcelona ya Hispania, Neymer ameomba mpango huo usitishwe kwa sasa hadi mchezo wa Super Cup upite.
Licha ya kuwa Neymer ni mgonjwa na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili lakini ameiomba klabu yake imuongezee wiki moja ya ziada kabla ya kurejea uwanjani na amependekeza Pedro asiondoke hadi mchezo wa Super Cup kati ya FC Barcelonadhidi ya Sevilla umalizike.
Mchezo huo utapigwa Jumanne ya August 11 utazikutanisha timu hizo ambazo ni washindi wa makombe ya Ulaya, Sevilla wakiwa wametwaa kombe la UEFA EUROPA LEAGUEhuku FC Barcelona ikiwa imetwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hata hivyo Pedro atajiunga na klabu ya Manchester United baada ya FC Barcelonakufikia makubaliano ya ada ya uhamisho wa pound milioni 22.3, Pedro anaondoka FC Barcelona baada ya kuwa hapati nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza mara kwa mara toka awasili Luis Suarez
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN


Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.