Kweli Dunia ina mambo, na ukichelewa kufa utakutana na mambo mwengi ya Dunia. Mwanamke mmoja nchini Marekani alichukuwa maamuzi magumu ya mchoma moto mpenzi wake katika sehemu zake nyeti baada ya kugundua kuwa anasalitiwa.
Habari zinasema kuwa mwanamke huyo aligundua sikunyingi sana kuwa mwanaume wake anamsaliti kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mfanyakazi wake, lakini aliamua kukaa kimya huku akifikiria nini cha kufanya ili kukomesha kabisa tabia hiyo ya usaliti wa kimapenzi. Na baada ya muda alipata jawabu na ndipo alipoamuwa kuchukuwa maamuzi hayo mazito.
Habari zinaendelea kunyetisha kuwa, mwanamke huyo alisubiri mwanamme wake akiwa amelala na kupitiwa kabisa na usingizi, ndipo alipomnyatia taratibu na kufunua shuka aliyokuwa kajifunika mwanamme wake kama inavyoonekana kwenye Picha hapo juu.
Baada ya kumfunua shuka hilo, alichukuwa aina fulani ya mafuta yawakayo na kuyamimina katika sehemu za mbele za mwanaume wake huyo aliyekuwa kalala huku kavaa nguo ya ndani (boxer) na socks, alihakikisha anamimina sehemu ambazo anajua sehemu za siri za mwanaume wake zimeelekea. na yote haya aliyafanya huku akiwa ametegesha kamera na kurikodi kila alichokuwa anakifanya.
Baada ya kuhakikisha kuwa mafuta hayo yalisha sambaa vizuri katika sehemu hizo, alichukuwa moto na kuugusisha katika mafuta yale aliyoyamwagia katika sehemu za siri za mwanaume huyo na ghafla moto ukaanza kuwaka kwa kasi.
Akiwa hajui hili wala lile mwanamme huyo alianza kuhusi sehemu zake za siri zikipata moto na ghafla akahisi kuungua...
alikurupuka na kuanza kujipigapiga katika sehemu zake nyeti ili kuuzima moto huo uliokuwa unaendelea kumuunguza. aliendelea kujipigapiga na huku akisindikizwa na matusi kutoka kwa mpenzi wake huyo aliyekuwa sasa anamwambia sababu ya yeye kuchukua maamuzi hayo.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN






Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.