MO |
ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA...
Alirudi chumbani na kwenda kuendelea na shuguri zake.
huku sebuleni Mzee Bisu aliendelea kutafakari ni jinsi gani ampate mfanyakazi wake huyo ambaye tayari ameuteka moyo wake. akajipa ujasiri na kuamua kufanya jambo...
SASA ENDELEA...
Alijiweka vizuri pale kwenye sofa kisha akajikohoza kidogo akaanza kuita.
"... Hasina... Hasina..."
huku chumabani Hasina aliisikia sauti ya boss wake ikimuita, akavaa nguo harakaharaka kisha akiitika pia kwa isauti.
"... Bee baba..."
"... Njoo mara moja..."
alimalizia mzee Bisu huku akijiweka vizuri pale kwenye sofa. mara mlango wa chumba cha Hasina ulifunguliwa na Hasina akatoka akiwa amevalia lile ligauni lake la kila siku.
alisogea mpaka jirani na pale alipokaa mzee Bisu akasimama kwa heshima zote.
"... Bee baba..."
mzee bisu aligeuza shingo na kumuangalia, alijikuta akikunja uso wake baada ya kukuta kuwa Hasina alikuwa kavaa tena kile kinguo ambacho hakioneshi kabisa mwili wake ulivyo.
alimuoneshea kwa alama ya kidole huku akimwambia kwa sauti nzito.
"... kaa hapa..."
Hasina alisogea taratibu na kukaa kwenye sofa huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio, alikuwa akijiuliza ni kitu gani alichoitiwa kwani hata siku moja hakuwahi kukaa na boss wake huyo kama walivyokaa siku hiyo. alikuwa akihisi kuwa labda kuna kosa alilifanya, lakini kila akitafakari kosa aliloliFanya hakuliona.
mzee Bisu naye kwa upande wake, alikuwa akitafakari ni jinsi gani aanze kumuingia mfanyakazi wake huyo aliyeupagawisha moyo wake ghafla. baada ya kutafakari kwa muda kidogo akapata ni wapi pa kuanzia.
"... Hasina,.." alianza kuongea huku macho yake yakiendelea kuwa kwenye luninga iliyokuwa mbele yake.
"... bee..."
Hasina aliitika kwa sauti ya upole.
"... hivi wewe huna nguo nyingine zaidi ya hilo gauni lako?.."
aliuliza swali la kizushi.
"... nguo zingine ninazo lakini sio nzuri..."
alijibu Hasina huku akivivunjavunja vidole vyake.
"... ina maana gauni hilo ndo zuri kuliko nguo nyingine zote ulizonazo?..."
"... hapana ziko nyingine zuri kidogo lakini zimechanika..."
mzee bisu alikaa kimya kwa muda kisha akajiweka sawa pale kwenye sofa na akawa kama anamsogelea kidogo.
"... sasa sikiliza Hasina... kesho nataka twende wote sehemu nikakununulie nguo zuri ili na wewe upendeze sawa?.."
aliongea mzee bisu kwa sauti ya taratibu na nzito kidogo. hasina alikubali tu kwa kichwa na huku macho yake yakiendelea kuvitazama vidole alivyokuwa akiendelea kuvivunjavunja.
"... unasikia Hasina wewe ni msichana mzuri na unatakiwa uvae vizuri ili usichana wako uonekane, usiwe unavaavaa vinguo vichafu kama hivyo wakati wewe nimsichana mzuri sawa?.."
Hasina alitabasam na huku akiendelea kukaa kama vile alivyokuwa akajibu.
"... sina zingine ndio maana na vaa hivi..."
"... sasa usijali kesho utakuwa mpya saw Hasina?.."
"... sawa baba..."
"... sasa sikia..." aliongea mzee bisu huku akiinuka kutoka pale kitini alipokuwa na kumfuata Hasina pale alipokaa, alikaa kwenye mkono wa sofa sehemu ile ya kuwekea mikono kisha akamshika mabegani.
"... sikia,.. wewe unasimu?.."
alimuhoji huku akimpapasa taratibu mabegani.
"... sina..." alijibu hasina kwa sauti iliyojaa kitetemeshi.
"... basi kesho ntakununulia na simu... lakini usimuambie mtu yoyote yule humu ndani sawa?.."
"... sawa..."
"... hata hizo nguo nikikununulia usiseme kama mimi ndo niliyekununulia sawa?.."
"...sawa... "
alijibu tena Hasina na huku akijaribu kujitoa mikononi kwa mzee bisu.
USIKOSE KUJUA NINI KITAENDELEA KATIKA TOLEO LIJALO
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN