Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF August 18 kupitia kwa afisa habari wa shirikisho hilo Baraka Kizuguto imethibitisha kumkosa mshambuliaji wa kimataifa waTanzania anayecheza katika klabu ya Mansfield Town inayoshiriki Ligi daraja la tatu Uingereza Adi Yussuf.
TFF imethibitisha kumkosa mshambuliaji kwa sababu amepata majeruhi hivi karibuni hivyo klabu yake ya Mansfield Town imeomba kutojumuishwa kwa mshambuliaji huyo katika kikosi cha Taifa Stars kitakachosafiri August 22 kuelekea Oman kwa ajili ya mechi ya kirafiki kabla ya kwenda kuweka kambi Instabul Uturuki kwa kambi ya maandalizi zaidi ya mechi ya kufuzu AFCON 2017.
Adi Yussuf ambaye alitangazwa kuitwa katika kikosi cha Taifa Stars alizaliwa February 20 1992 visiwani Zanzibar lakini amewahi kucheza pia katika klabu ya Leicester City.Sambamba na hayo TFF imetangazwa kufungwa kwa dirisha la usajili siku ya Alhamisi ya August 20 na timu itakayoshindwa kumaliza usajili ndani ya wakati italazimika kulipa Tsh laki 5.
“palikuwa na mshambuliaji Adi Yussuf ambaye anacheza Mansfield Town ya Ligi daraja la tatu nchini Uingereza mwalimu alimuita kwa ajili ya kujiunga na kikosi chake taratibu zilifanyika za mchezaji huyu na alikuwa aungane na timu itakapokuwa kambini nchini Uturuki lakini katika mchezo aliocheza mwishoni mwa wiki alipata majeruhi”>>>Kizuguto
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN


Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.