Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

YANGA KWAFUKUTA...MILIONI 200 ZA BOSSOU ZAZUA BALAA....

01-Yanga
Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam
BALAA kubwa limeibuka katika kikosi cha Yanga ikiwa ni siku chache tu baada ya uongozi wa klabu hiyo kumsainisha beki wa kimataifa kutoka nchini Togo, Vincent Bossou.
Juzi Jumatatu, baadhi ya wachezaji wa timu hiyo waliujia juu uongozi wao na kuutaka uwalipe fedha zao za usajili wanazodai, vinginevyo hawataingia uwanjani kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC itakayochezwa Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimedai kuwa, wachezaji hao wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa usajili wa Bossou klabuni hapo umegharimu zaidi ya dola 100,000 (zaidi ya Sh milioni 200), jambo ambalo wameona siyo sawa kwa sababu uwezo wake uwanjani ni wa kawaida sana ukilinganisha na mabeki wengine wa timu hiyo.
“Wachezaji hao wanaidai Yanga fedha zao za awamu ya pili ya usajili wao ambazo walitakiwa kuwa tayari wameshalipwa mpaka sasa, lakini wamekuwa wakizungushwa. “Hata hivyo, jana (juzi) wameutaka uongozi uwalipe fedha zao haraka iwezekanavyo vinginevyo hawatakuwa tayari kuingia uwanjani kucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam na kama watawalazimisha basi watacheza chini ya kiwango.
“Hata hivyo, jambo ambalo limewafanya wafikie hatua hiyo ni baada ya kupata taarifa ya kiasi cha fedha za usajili wa Bossou ambazo zinadaiwa kuwa ni zaidi ya dola 100,000.
“Hakika taarifa hizo ziliwaumiza sana na hata nilipokuwa nikizungumza nao walionyesha kutofurahia hali hiyo kwani wanadai kuwa ni fedha nyingi sana alizopewa, bora fedha hizo zingetumika kwa ajili ya kulipa madai yao hayo,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha ili aweze kulizungumzia suala hilo hakuweza kupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita tu bila ya kupokelewa na baadaye akatuma ujumbe mfupi kuwa yupo kwenye kikao.
Hata hivyo hali iliyojitokeza pia kwa mkuu wa kitengo cha habari wa klabu hiyo, Jerry Muro ambaye simu yake ilikuwa haipokelewi.
Baadhi ya wachezaji wanaodaiwa kutaka kugomea mechi hiyo mpaka watakapolipwa fedha zao ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Ally Mustafa ‘Barthez, Deogratius Munishi ‘Dida’, Pato Ngonyani, Juma Abdul, Said Makapu, Salum Telela na Simon Msuva

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top