Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

RAIS MAGUFULI KAAMUA BILIONI ZLIZOKUWA ZITUMIKE SIKUKUU YA UHURU ZIFANYE KAZI IFUATAYO...

Kwa sababu tayari Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza kwamba sherehe za Uhuru siku ya December 09 2015 hazitokuwepo, ninayo taarifa nyingine kuhusu maamuzi mengine ya pesa ambazo zilitengwa kwa shughuli hiyo.
Taarifa kutoka Ikulu imetolewa kwamba fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya kutumika kugharamia sherehe za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika December 09 2015, zitumike kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco iliyopo Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia za barabara za lami.
Taarifa hiyo ya Ikulu imesema tayari fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.
Hii hapa taarifa yote ya Ikulu.
IMG-20151130-WA0042
Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kubadilisha matumizi ya pesa, kama unakumbuka siku alipolihutubia Bunge November 20 2015 aliagiza zaidi ya Milioni 200 zipelekwe kununulia vitanda vya wagonjwa hospitali ya Muhimbili badala ya kutumika kwenye sherehe za Wabunge Dodoma

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top