Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

DONALD NGOMA, KAMUSOKO WATENGWA YANGA SC...


Donald-Ngoma-12Donald Ngoma.
Sweetbert Lukonge, Zanzibar
KILA lenye mwanzo lina mwisho wake, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya wachezaji wawili wa kimataifa wa Yanga, Wazimbabwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko kutengwa klabuni hapo.
Hivi sasa wachezaji wao kila moja wao anapofunga bao, wamejikuta wakishangilia peke yao bila ya kupata sapoti ya wenzao. Wamekuwa wakishangilia kwa staili ya kushikana mabega huku wakiwa wameunganisha vichwa vyao na kuinama kidogo.
Siku za hivi karibuni staili hiyo ya ushangiliaji wa wachezaji hao ilizua gumzo jijini Dar es Salaam kutokana na kujadiliwa mara kwa mara katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Hata hivyo, visiwani hapa pia iliibua gumzo kwa mashabiki wa soka siku ambayo Ngoma aliiwezesha Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 ilipocheza dhidi ya Mafunzo FC ambapo walishangilia kwa staili hiyo, hali iliyosababisha wachezaji hao kutengwa na wenzao.
kamusokoAkizungumza na Championi Jumatatu jana,  mmoja wa wachezaji wa Yanga ambaye aliomba kutotajwa jina lake gazetini, alisema kuwa wamefikia hatua hiyo ili kuepukana na balaa la kuchafuliwa katika mitandao ya kijamii na watu wenye upeo mdogo na mitazamo michafu.
“Hivi sasa kila wanapofunga sisi tunashangilia nao kama kawaida lakini ile staili ya kushikana mabega na kuunganisha vichwa huku tukiwa tumeinama tumewaachia wenyewe.
“Tumekuwa tukichafuliwa sana katika mitandao ya kijamii hivyo tumeona tuwaachie wao ila sisi tutakuwa tukishangilia nao kawaida mpaka hapo watakapokuwa wamepata staili nyingine,” alisema mchezaji huyo.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top