MAMLAKA ya udhibiti wa mawasiliano nchini (TCRA) imekitoza kituo cha redio cha Clouds FM faini ya shilingi milioni 12 ikiwa ni pamoja na kupewa onyo kali kwa sababu ya kukiuka maudhui na kanuni za utangazaji kupitia vipindi vya Jahazi na XXL
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema Clouds FM imetozwa shilingi milino tano kwa kosa la kukiuka misingi na maudhui ya utangazaji kupitia kipindi cha Jahazi kwenye kipengele cha Mastori ya Town, shilingi milioni tano kupitia kipindi cha Jahazi kipengele cha Najua Wajua na shilingi milioni mbili kupitia kipindi cha XXL.
“Hata hivyo, tunaitaka Clouds Media Group kuwaomba radhi wasikilizaji wa vipindi hivyo kwa siku tatu mfululizo na pia tunautaka uongozi wa Clouds Media Group kuwachukulia hatua za kinidhamu watangazaji wanaokiuka maadili, miiko na kanuni za utangazaji,” alisema Mapunda.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.