Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

AJALI YA NDEGE UKRAINE... IRAN ILIDUNGUA NDEGE HIYO KIMAKOSA?..

Ndege iliyopata ajali Iran na kuuwa watu 176, ilikuwa inajaribu kugeuza na kurudi uwanja wa ndege wakati ajali hiyo ilipotokea, uchunguzi uliofanywa Iran umesema.
Ndege aina ya Boeing 737-800 ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari kutoka uwanja wa ndege wa Tehran, na hakuna mtu yeyote aliyeweza kupona.
Upelelezi uliofanywa umebaini kuwa ndege ilikuwa na itilafu wakati inaaza safari yake, na moto ukaanza kushika.
Awali Iran ilisema kuwa haitakabidhi kisanduku cha kunakili safari ya ndege ama ''Black box'' ya ndege ya Ukraine iliyopata ajali na kuua watu 176, kwa kiwanda kilichotengeneza ndege hiyo au kwa Marekani.
Ndege hiyo ya Ukraine aina ya Boeing 737-800 ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari yake kutokea uwanja wa ndege wa Tehran, na hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo.
Kwa mujibu wa sheria za anga za kimataifa , Iran ina haki ya kufanya uchunguzi kuhusu ajali hiyo.
Lakini watengenezaji wa ndege hiyo kwa ushirikiano na wataalamu kutoka nchi kadhaa wanaweza kuchunguza kisanduku hicho.
Ajali hiyo imetokea wakati ambapo kuna mvutano mkubwa kati ya Marekani na Iran, muda mfupi baada ya Iran kushambulia kwa makombora kambi mbili za kijeshi za Marekani zilizopo Iraq.
Aidha hakuna ushahidi kuwa matukio haya mawili yanahusiana na kuanguka kwa ndege hiyo.
Kwa kawaida, bodi ya Marekani ya usafirishaji salama ina jukumu la kuchunguza masuala lolote la kimataifa linalohusisha ndege aina ya Boeing iliyotengenezwa Marekani kwa idhini ya sheria za nchi husika.
Kiongozi wa shirika la anga Iran Ali Abedzadeh alinukuliwa katika vyombo vya habari nchini humo akisema:"Hatutawapa kisanduku cheusi kampuni iliyotengeneza ndege hiyo au Wamarekani"
"Tukio hilo litachunguzwa na shirika la anga la Iran lakini Ukraine itaruhusiwa kuepo katika uchunguzi huo," aliongeza.
Bwana Abedzadeh alisema kwamba hana uhakika ni nchi gani zitaweza kufanyia uchunguzi wa kisanduku hicho cheusi kinachotunza sauti zilizonaswa katika ndege.
Shirika la Boeing lilisema kuwa liko tayari kusaidia kwa namna yeyote itakayoitajika, wakati huohuo waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau alisema kuwa alitarajia nchi yake ina wajibu wa kufanya uchunguzi kuhusu ajali hiyo na iko tayari kutoa msaada wowote wa kiufundi.
Ndege ya kimataifa ya Ukraine nambari PS752 iliyokuwa inaelekea Kyiv ilikwa na watu 176 wakati inaanguka siku ya jumatano.
Abiria wengi walikuwa raia wa Iran na Canada.
Mara tu baada ya ajali, Ubalozi wa Ukraine uliopo Tehran ulilaumu itilafu za kiufundi na kudai injini ya ndege kushindwa kufanya kazi na ndio chanzo cha ajali hiyo lakini baade ilikanusha tamko lake na kudai kwamba halikuwa rasmi.
Wakati ndege ilipoanguka karibu ya mji mkuu wa Iran, haikuonekana vizuri , kwa mujibu wa mtandao wa Flightradar24 . Maafisa wa shirika la ndege walieleza.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa angalizo la watu kuwa makini na "uvumi na majibu ya nadharia kuhusu janga hilo" mpaka taarifa rasmi zitakapotangazwa.
Vyombo vya habari vya Iran vimelaumu itilafu za kiufundi na kumnukuu afisa wa masuala ya usafiri wa anga ambaye alisema kuwa hakuna taarifa ya dharura iliyosemwa.
Huku bwana Abedzadeh alisema "ugaidi" unahusika katika ajali hiyo.
Nani walikuepo katika ndege hiyo?

Kulikuwa na abiria 82 wa Iran, 63 wa Canada, 11 Ukraine pamoja na wafanyakazi 11 wa ndege, 10 Sweden, wanne Afghanstan, watatu Britons na watatu Wajerumani, alibainisha waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Vadym Prystaiko. Kumi na tano kati ya waliokufa ni watoto.
Lakini serikali ya Ujerumani ilisema baadae kuwa hawana uhakika kama raia wa Ujerumani walikuwa katika ndege hiyo iliyopata ajali Iran.
Presentational white space
Mkuu wa kitengo cha dharura cha Iran amesema kuwa abiria 147 walikuwa Wairan. Hivyo ni raia 65 tu ndio wametoka mataifa ya kigeni au wana uraia wa nchi mbili.
Bwana Trudeau alisema kuwa abiria 138 katika ndege hiyo walikuwa wanaelekea Canada na kupitia njia ya Kyiv.
"Watu wote waliokuja nyumbani kuona wazazi wao, marafiki zao, wafanyakazi wenzao au familia zao," alisema. "Wote walikuwa na uwezo mzuri wa maisha ya baade ".
Taarifa kuhusu ndege hiyo zilibainishwa katika mtandao kuwa ndege ilipaa vizuri angani kutoka Tehran.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top