Enzi hizi kipindi cha mababu zetu na katika tamaduni za muafrika neno Ndoa ilikuwa ni kitu kilichokuwa kikichukuliwa kwa uzito mkubwa sana tofauti na ilivyo kwa sasa. Babu zetu walikuwa wanaheshimu sana kitu kinachoitwa Ndoa, kulikuwa na mipaka iliyokuwa inazuia watu kuoana.
katika enzi hizo ilikuwa hairuhusiwi ndugu kuoa katika ukoo moja, ilikuwa pia hairuhusiwi mtu kuoa mtu ambaye wanatoka katika koo moja, ilikuwa ni vigumu kwa mtu kuoa dada wa tumbo moja au hata binamu ilikuwa sio rahisi.
Lakini katika kizazi hiki cha sasa, vitu na mambo ya ajabuajabu hutokea tu, tena vitu ambavyo kwa mababu zetu havikuwahi kutokea.
Mapacha hawa wanaofanana waliamua kufanya kitu ambacho hakikuwahi kutokea kwa enzi za mababu zetu ambapo waliamua kuolewa na mwanaume mmoja na kuishi naye kwa furaha kabisa bila shida.
Olwethu na Owami, ni mapacha wanaofanana wanaoishi nchini South Africa, walilelewa na Babu na Bibi yao na walipokuwa walikuta wakiwa katika sanaa ya uigizaji katika vipindi mbalimbali vya Television mbalimbali huko South Africa.
Walipoamua kuolewa na mwanamme mmoja wote walisema kuwa walijikuta katika mapenzi ya dhati na mwanamme huyo hivyo kwa pamoja wakaamua kuolewa naye. lakini ajabu ni kuwa waliishi kwa miaka michache tu baada ya kuamua kutalikiana na mwanaume huyo.
baada ya kumtaliki mume wao, mapacha hao walikiri kuwa wanajuta kuolewa na mwanaume huyo na kwa sasa wako katika msako wa kumtafuta mwanamume mwingine atakaye waoa wote wawili kwa pamoja kwani hawataki kuolewa na wanaume tofauti, wao lengo ni wapate mwanaume mmoja tu na bado wanamatumaini kuwa watampata.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.