Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

KITOTO KICHANGA CHAKUTWA KIMEKUFA NDANI YA MFUKO WA RAMBO

Katika hali ya kushangaza na ya kusikitisha, kitoto kichanga kimekutwa kimetupwa kikiwa kimefungwafungwa ndani ya mfuko wa rambo.
habari za kuaminika na zilizoshuhudiwa na MO Designtz zinasema kuwa kitoto hicho ambacho akijulikani nani amekitupa kilikutwa katika viunga vya nyumba za kota zilizobomolewa maeneo ya magomeni Tanesco tena jirani kabisa na ofisi za Tanesco Magomeni.
Habari hizo zinasema kuwa kitoto hicho kilikutwa tayari kimeshakufa na kina kadiriwa kuwa ni kati ya miezi 6 au 7. Watu wengi walifurika kukishuhudia huku wengi wao wakiwalaani wanawake wenye tabia na roho chafu kama za huyo aliyekitupa kitoto hicho.

KITOTO KILICHOTUPWA KIKIWA NDANI YA MFUKO WA RAMBO
Habari za kuaminika zinasema kuwa kitoto hicho kiligunduliwa leo Alhamisi mida ya saa nane na robo mchana ( 14: 15) na mmoja wa waokota makopo aliyekuwa anapita maeneo hayo akiwa katika Shughuli zake za kuokota makopo . aliuona mfuko ukiwa umefungwa akaenda kuukagua akitegemea kupata kopo lakini akakutana na kitoto hicho kikiwa tayari ni maiti, alichokifanya ni kupiga kelele na watu wakasogea kuangalia nini kinaendelea.

BAADHI YA WATU WALIOJITOKEZA KUKISHUHUDIA KITOTO HICHO
Simu ilipigwa polisi baada ya watu kizidi kufurika kukishuhudia kitoto hicho na ndipo polisi wakawasili na kukichukuwa kichanga hicho na kuondoka nacho. Habari za kipolisi zina sema kuwa watalishughulikia swala hilo ili kubaini ni nani aliyefanya ukatili huo ili muhusika akalipe sawasawa na uovu wake.
kumekuwa na matukio mengi sana ya aina hii yakijitokeza katika jamii zetu, na hii inaonesha ni jinsi gani watu wengi wamekuwa roho za kinyama na kukosa kabisa utu. "... kwa mtu mwenye imani na roho ya utu hawezi akachukuwa hatuwa kama hii, huu ni unyama uliopitiliza, kwa sababu kiki ni kiumbe kabisa... mtu utu aliyefanya hivi ni sawasawa na muuaji na hukumu yake haiwezi kutofautiana na hukumu ya muuaji..." alisema shuhuda mmoja aliyeonekana kuwa na sasira baada ya kuona tukio hilo

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top