Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

FAMILIA ZAIDI YA 200 ZAACHWA BILA MAKAZI ZANZIBAR KWA MAFURIKO...


Familia zisizopungua 200 zimeachwa bila makazi baada ya makazi yao kuharibiwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyoikumba manispaa ya mji wa Unguja na Vitongoji vyake.
Akizungumza kwa njia ya simu mkazi mmoja wa Mwanakwerekwe sokoni, Mjini Unguja ndugu Mussa Makame, alisema kuwa mvua hizo zilizoendelea kwa siku mbili mfululizo, zimepelekea maafa makubwa katika miundombinu mjini humo.
"hali ya hewa Zanzibar kwa sikumbili mfululizo imekuwa na utata wa hali ya mvua na maafa mengi yameyokea" alisema ndungu Mussa Makame na kuongeza kuwa kunataarifa ambazo hazijathibitishwa za watu wawili kupoteza maisha kutokana na mvua hizo na kwamba vyombo vinavyohusika vitatoa tamko rasmi kuhusiana na tetesi hizo.
akaendeleea kusema kuwa wananchi wamekuwa wakishirikiana katika juhudi za kusaidia waathirika wa janga hilo na kwamba serikali imetenga makaazi ya muda katika mashule na kujenga mahema kwaajili ya kuzihifadhi familia zilizoathirika na janga hilo.
aliyataja maeneo yaliyoathirika zaidi kuwa ni Mwanakwerekwe, Jang'ombe, Chumbuni na tomondo.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top