Juzikati wasanii Baraka Andrew ‘Barakah da Prince’ na Estelina Sanga ‘‘Linah’ walinaswa wakiwa kimahaba, tukio lililoibua gumzo na wengi kudhani mkali huyo wa ngoma ya Siwezi tayari kachepukia kwa ndege mnana.
Barakah da Prince na Linah.
Baraka na Linah walinaswa katika viunga vya Escape One kulikokuwa na shoo ya Christian Bella ambapo jamaa alionekana akimshikashika mdada huyo bila aibu.
Akilifungukia tukio hilo, Baraka alisema kuwa, yalikuwa ni mapozi ya kawaida tu na wala watu wasihisi anachepuka na Linah.
“Hivi nimsaliti Naj (Najma mpenzi wake wa sasa) sijipendi? Yale ni mapozi ya kawaida tu. Narudia tena, nampenda sana Naj na hakuna mbadala wake,” alisema Baraka.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.