
Habari: na Daniel Micho Mulume MO Design DRC
Mamia ya Raia na Wakazi wa Mji wa Goma huko Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wameamua kuingia mabarabarani na kuandamana, kupinga harakati za Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila kuwania tena awamu ya tatu ya urais.
Maandamando hayo yalipelekea mshikemshike mkubwa ambapo polisi na Raia waliingia katika mvutano na kusababisha kifo cha raia mmoja na wengine wengi kuumizwa.
Taarifa zinasema kuwa raia aliye fariki dunia alijifyatulia risasi akiwa katika harakati za kugombea silaha kati yake na polisi.

Maandamano hayo ambayo inasemekana yalikuwa ya vurugu kwa raia kufunga mabarabara kwa kujaza mawe na kuchoma moto mabarabarani yalipelekea raia takriban 35 kutiwa nguvuni kulingana na vurugu hizo za kumpinga Rais Joseph Kabila kutumikia awamu nyingine ya Urais wa nchi hiyo.

Pamoja na harakati zote za raia hao kuandamana kwa hali hiyo ya vurugu na vitisho, lakini uongozi upande wa serikali umesema kuwa hizo ni kelele za chura tu na haziwezi kumzuwia Ng'ombe kunywa maji, kwani maandamano yamefanyika na harakati zinaendelea. inasemekana kuwa walioandamana sio watu kamili bali vijana wamitaani (ikimaanishwa wahuni tu).

Rais Joseph Kabiala ni Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo DRC, ambapo kwa wakati huu anatumikia awamu ya pili ya Urais wake toka aingie madarakani. kama ilivyokuwa alipotaka kugombea awamu ya pili kulitokea na vurugu kama hizi, na sasa anataka tena kugombea awamu ya tatu.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.