PARIS, Ufaransa
TIMU ya taifa ya Ufaransa inafungua pazia la michuano ya Euro 2016 leo Ijumaa katika mtanange dhidi ya Romania huku ikiwa inapewa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa ubingwa wa mwaka huu. Mechi ya leo itaanza majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Timu nyingine zilizopo kwenye kundi moja na Ufaransa, ukiachana na Romania, ni Albania na Uswisi.
Kuelekea mchezo wa leo, Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps, amesema: “Nawaamini wachezaji wangu. Mechi ya kwanza siyo ya kuamua lakini ni muhimu kwa sababu inatengeneza morali ya mechi zote.”
Timu yaRomania
Romania wanaonekana kuhangaika katika kufunga mabao lakini ukuta wao ni mgumu kupitika. Hatari kubwa ya Ufaransa ni katika ulinzi baada ya Raphael Varane na Lassana Diarra kuwa majeruhi. Laurent Koscielny na Adil Rami, wanaonekana ndiyo watakaochezeshwa leo katika ukuta wa kati lakini ni mara chache wamecheza pamoja na walipocheza walionyesha kutokujiamini na makosa kibao.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.