Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

MWANZA: MUUAJI MSIKITINI AWATOROKA POLISI KIKOMANDO...


Gazeti la Nipashe July 5 Limeripoti habari hii kutoka Mwanza, kuwa Muuaji mmoja aliyeua Msikitini alifanikiwa kuwatoroka Polisi.
Gazeti hilo limeripoti kuwa jeshi la polisi mkoani Mwanza limesema mtuhumiwa wa ujambazi waliyemkamata kwa matukio mbalimbali ya uhalifu yakiwamo ya uporaji maduka ya miamala ya kifedha na mauaji ya watu watatu msikitini, Hamis Juma, ametoroka chini ya ulinzi mkali wa polisi wakati akiwapeleka mlimani kuwaonyesha wahalifu wenzake.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Ahmed Msangi alisema juzi mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Nyegezi, alikuwa mikononi mwa polisi akiwapeleka walipojificha wenzake katika mlima Kiloleli Nyasaka kata ya Kirumba wilayani Ilemela.
Msangi alisema baada ya polisi na mtuhumiwa huyo wa ujambazi kufika eneo la tukio saa 8:00 usiku ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika mlima huo walianza kurusha risasi kwa askari ambao walitaharuki na kujibu mashambulizi huku wakimsahau mtuhumiwa aliyewapeleka ndipo alipopata mwanya wa kutoroka.
Aidha alisema katika mapigano hayo, polisi walikamata bunduki aina ya shortgun iliyokatwa mtutu na kitako na risasi moja kwenye chemba iliyotupwa na majambazi hao.
Unaweza kuzipa habari hizi pia kwenye magazeti ya July 05 2016

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top