
Beki wa kati wa klabu ya Manchester United ya England ambaye pia anachezea timu ya taifa ya England Chris Smalling jina lake limeingia kwenye Kurasa baada ya kuanguka na kupasuka sehemu ya juu ya jicho la kulia akiwa katika mapumziko yake nchini Indonesia.
Kwa mujibu wa mitandao mikubwa ya habari duniani kama dailymail na mingine, imeripoti kuwa Smalling kuanguka na kupasuka sehemu ya jicho la kulia ni baada ya kula chakula ambacho kinatajwa kuwa kilikuwa na sumu.

Smalling alikuwa mbali na mpenzi wake Sam Cooke na alianguka na kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu, beki huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa sasa kichwani kwake kawekwa bandeji kutokana na kuumia sehemu ya juu ya jicho la kulia.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.