DUNIA ina maajabu! Mwanamke mmoja (jina halijajulikana mara moja) amejikuta akivunja ndoa yake ya wiki moja baada ya picha zake za utupu akijiachia ‘kimalovee’ na boyfriend wake wa zamani kumfikia mume wake wa ndoa wakati wakiwa fungate (honey-moon) baada ya ndoa yake na mumewe iliyofanyika jijini Dar es Saalam.
Tukio hilo la aibu limetokea wiki moja tu baada ya wawili hao kufunga pingu za maisha. Kupitia ujumbe wa sauti mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo alijipiga na mpenzi wake zamani miaka saba iliyopita wakiwa chuoni.

“Ni kweli ni mimi ndiye niliyepiga hizo picha lakini ni muda mrefu tangu kipindi nikiwa chuo, yaani hata huyo mtu mwenyewe sijui yuko wapi sina mawasiliano naye tena, sikutegemea kiukweli,” anasema mwanamke huyo.

“Mpaka sasa hivi sijui nafanya nini.”
Kwa upande wa mume wake, alidai kuwa picha hizo zimeuvunja moyo wake.
“Tulikuwa tumeshaenda kwenye honey moon tumerudi, sikuamini macho yangu baada ya kuona hizo picha na huyu mwanamke, rafiki zangu walikuwepo wengi sana, best man wangu pia ni vitu ambavyo kuvizungumza mimi nashindwa, naanzia wapi, lakini mapenzi huwa yako hivyo, inawezekana iko hivyo lakini sasa kama mazingira kama yale hata kama ukiwa ni wewe lazima utaumia, familia yangu ntaiambia nini mimi, imenigharamia harusi kubwa,” alisema mwanaume huyo.
Amedai kuwa haoni kama inawezekana tena kukaa chini na mke wake huyo kwa kile kilichotokea.
“Nikae chini ili iweje?” alihoji kwa jazba. “Imeniuma, imeniumiza sana hii kitu haki ya Mungu, hata kama miaka kumi imepita kwanini imekuja kwenye harusi yangu, zawadi zimekuja kwaajili ya harusi yetu kwanini aletewe picha za aina hiyo? Angeniambia before kwamba nilikuwa na moja mbili, ningekuwa najua, lakini amenificha. Imenicost kwa kiasi kikubwa sana, nitaiambiaje familia yangu kwa mfano? Nitasema nini.”

“Sitokuja kupenda tena mwanamke wa aina yoyote ile, mpaka nakuja kuingia kaburini, I swear to God, imetosha kabisa.”
Wawili hao walifunga ndoa tarehe April 23 mwaka huu.
Sikiliza maelezo kamili ya mwanamke huyo hapo chini
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.