
Habari na Daniel Michombero - Congo DRC
Ofisi ya Jeshi la Taifa FARDC katika mji wa Goma DRC au Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeungua moto na na kuteketeza kila kilichokuwemo ndani ya ofisi hiyo, MODesign tumeipata kupitia mwandishi wetu aliyeko DRC.

Habari zinasema kuwa huo ulioshindika kuzimwa na magari ya zimamoto ulitokana na itilafu ya umeme ulioanzia kwenye waya wa umeme katika ofisi hizo.
Akizungumza kwa masikitiko msemaji wa jeshi hilo Bwana Guillaume Njike Kauko, alisema kuwa vitu vingi na vyenye thamani kubwa viliungulia ndani ya ofisi hiyo ikiwa ni pamoja na macomputer, mafaili yenye nyaraka mbalimbali za kijeshi na vitu vingine vingi.

Habari zinasema kuwa tukio hili lililotokea Jana majira ya saa kumi na mbili (12) jioni liliacha masikitiko kwani mpaka magari ya zimamoto yalishindwa kabisa kuuzima moto huo, na magari yaliokuwepo katika kuzima moto huo ni yale ya Taifa pia na Yale ya Monusco hayakufua dafu.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.