Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

IKO HAPA VIDEO YA ASKARI AKIPOKEA RUSHWA LAIVU...



Askari Polisi aliyetambulika kwa jina moja la AFANDE ALLY wa mjini ZANZIBARI ameonekana kwenye video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba na kupokea RUSHWA ya shilingi za KITANZANIA 60'000 kutoka kwa mmoja wa MTALII ambaye hakuweza kufahamika jina lake na NCHI aliyotokea.
TUKIO hilo limetokea maeneo ya MAHONDA mjini humo kipindi MTALII huyo akiwa akielekea BEACH ya NUNGWI, akiwa ameambatana na MWANAMKE mmoja ambaye ni MTANZANIA,ambapo AFANDE ALLY aliwasimamisha WATALII hao na kuwataka waonyeshe LESENI ya gari,lakini MTALII huyo hakuwa na LESENI.
ASKARI huyo alipogundua kuwa MTALII huyo hana LESENI,akaanza kumuomba RUSHWA ya shilingi 60000 huku akisikika kuwafundisha ujanja wa namna ya kuwakwepa ASKARI watakaokutana nao katika safari yao,kuwa waseme kuwa LESENI yao imeshikiliwa na POLISI kwa kosa la kuendesha gari pasipo kufunga mkanda.
Hata hivyo baada ya ASKARI huyo kupokea RUSHWA hiyo,MTALII huyo alisikika akisema kuwa hatorudi tena ZANZIBAR.
"Hii tabia ni mbaya sana kwa kweli  ,nikiondoka sitarudi tena  ZANZIBAR" alisema MTALII huyo kwa masikitiko huku akijiandaa kuondoka eneo hilo.




BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top