R.I.P Juliana,... yule Video queen aliyetamba kwenye video ya Salome ya Mwanamuziki wa Bongo fleva Nasib Diamond Platnumz ajulikanaye kama Juliana, ameuawa usiku wa kuamkia leo.
Habari zinasema kuwa Juliana alitekwa, akateswa, akabakwa na kisha kunyongwa mpaka kufa. Maiti ya juliana imeokotwa leo.
Juliana alikuwa na umri wa miaka 18 tu, ni mzaliwa wa arusha.
Huu ni msiba wa watanzania, lakini pia watanzania tujiulize maswali, ni wapi unakoelekea kwa matukio kama haya?..uko wapi utu?... mbona tumekuwa kama wanyama? iko wapi ile amani ambayo watanzania tunajivunia siku zote kama pia tutakuwa tunauwana kinyama kwa style hizi? Jana tulitoka kumzika Mashari aliyeuawa, lakini leo hi pia Juliana naye kauawa, ni nini hiki kimetupata watanzania?
MO Design tunalaani vitendo hivi na tunaiomba serikali isilifumbie macho hili, ihakikishe hawa watuhumiwa wanakamata na sheria ifuatwe.
R.I.P Juliana
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.