Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

RAIS MAGUFULI AWAGEUKIA WANAHABARI...

Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ametoa onyo kwa vyombo vya habari nchini humo kwa madai vinaandika habari zisizo za kizalendo.
Kiongozi huyo amemtaka waziri mpya wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe kuvichukulia hatua za kisheria.
"Kila kitu chenye nia ya uchochezi fulani fulani, wao ndio stori. Sasa Mwakyembe kafanye kazi. Nataka ukafanye kazi. Kama wapo waliokuwepo waliokuwa wanashindwa kuchukua hatua wewe kachukue," amesema Dkt Magufuli alipokuwa anamwapisha Dkt Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Dkt Magufuli pia alimuapisha Prof Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, na Bw Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu.
"Kwa kuwa wewe ni mwanasheria mzuri, msomi, umesomea mambo ya habari, kafanye kazi. Serikali ipo. Hatuwezi tukaiacha serikali ikaangamia kwa sababu ya wat wachache."
"Nchi yetu huko nje ina sifa kubwa sana, juzi tu hapa amekuja rais wa Benki ya Dunia na amekubali kutupatia Shilingi Trilioni 1.74 na pia Benki ya Dunia ipo katika mchakato wa kutupatia fedha zingine Shilingi Trilioni 2.8 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, haya ndiyo mambo muhimu ya kuandika lakini hebu angalia siku iliyofuata jinsi magazeti yalivyoandika," amesema Dkt Magufuli.
Rais Magufuli ameonyesha kuchukizwa na habari zilizopamba ukurasa wa juu katika magazeti ya leo ambapo magazeti mengi yameweka picha ya aliyekuwa waziri wa habari Nape Nnauye akitolewa bastola katika vurugu zilizotokea jana.
"Hata kasomeni tu leo magazeti ya leo. Picha yote heading ni picha ya mtu ambaye alifanya kosa moja, kana kwamba kitendo hicho kilifanywa na serikali. Kwanza ukurasa wa pili, huyu anatoa anafanya hivi....nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari, tahadharini. Kama mnafikiri mna uhuru wa namna hiyo, haujafikia huko."
KAMA HUJASIKIA NGOMA MPYA YA MUSSA SIKAWE DAMU TULIZA MOYO, HII HAPA

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top