Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

VITA YA SERIKALI NA MASAI SERENGETI - SERENGETI

Zaidi ya manyatta 100 za jamii ya Maasai zinadaiwa kuchomwa moto na mamlaka za mbuga ya wanyama pori karibu na mbuga ya wanyama pori ya Serenegeti.
Mamia ya watu wanaripotiwa kubaki bila makao kutokana na kuondolewa kwa jamii hii ya wafugaji. na Kijana mmoja wa kimasai anaripotiwa kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya.
Hii ni sehemu ya mzozo wa muda mrefu kati ya jamii ya Maasai na mamlaka ambazo huendesha shughuli za uwindaji kwa watalii.

Serikali ya Tanzania ina mipango ya kubuni eneo la ukubwa wa kilomita 1500 mraba kwenye mbuga hiyo, kwa kampuni yenye makao yake nchini Dubai ambayo hutoa huduma za uwindaji kwa watalii matajiri kutoka Milki ya nchi za kiarabu.
Mipango hiyo itasababisha watu 30,000 kupoteza makao na matatizo mengine kwa jamii ya Masai ambayo hutegemea malisho kwa mifugo wao.
Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwani Kerry Dukunyi amesema kuwa wanavijiji wamepoteza mali katika kisa hiki cha hivi punde.
"Kiwango kikubwa cha chakula chetu kimeharibiwa... Tumepoteza chakula kingi," alisema
"Mifugo kadhaa pia haijulikani iliko."

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top