Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

ODINGA: KENYATTA NI RAISI WA KOMPUTER... ATANGAZA KWENDA MAHAKAMANI...

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametangaza kwamba muungano wake wa National Super Alliance utawasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumanne wiki iliyopita.
Bw Odinga alikuwa amesema ingawa muungano huo ulikuwa umeapa kutowasilisha kesi kortini wakati huu, wameona ni heri kufanya hivyo "kufichua uovu uliotokea wakati wa uchaguzi mkuu."
"Tumeamua kwenda kortini kufichua jinsi uongozi wa kompyuta ulivyofanikishwa," amesema Bw Odinga akiwahutubia wanahabari mtaa wa Lavington, Nairobi.
"Hawa ni viongozi wa kompyuta. Kompyuta ndiyo iliwataga, kompyuta iliangulia, kompyuta iliwatoa. Vifaranga vya kompyuta."
Kiongozi huyo amesisitiza msimamo wa NASA kwamba uchaguzi haukuwa huru na wa haki.
Amesema mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC ilidukuliwa na matokeo kuvurugwa kumfaa Bw Kenyatta ambapo kulikuwa na pengo kiasi fulani kati yake na Bw Odinga muda wote wa kutangazwa kwa matokeo.
"Mtindo huu ulitokea pia katika maeneo mengi na kwenye uchaguzi wa ugavana. Jambo kama hili halijawahi kutokea katika uchaguzi wa kidemokrasia pahala pengine popote duniani. Lakini ilitokea hapa," alisema.
Bw Odinga amesema udukuzi huo una uhusiano na kuuawa kwa meneja wa teknolojia katika tume hiyo Chris Msando ambaye aliuawa wiki moja kabla ya uchaguzi.

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

Post a Comment

Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.

CodeNirvana
© Copyright MO Design
Back To Top