Welcome

    Featured Posts

    MO DESIGN

    Social Icons

Loading...

AINEA AMKALISHA SHETA NDANI YA SOMEBODY

AINEA Ft SHETA - SOME BODY
AINEA EMMANUEL, kidogo linakuwa kama jina geni kwa wapenda muziki wa Bongo flava, lakini ni kisema tu AINEA, wengi mtakuwa mnamfahamu, ni msanii wa BONGO FLAVA ambaye anaendelea kufanya vizuri katika mendani ya muziki huu wa kizazi kipya. AINEA sasa hivi anatamba na kibao kitwacho SOME BODY ambacho amekamua vikali kwa kushiriaana na SHETA. ngoma hiyo tayari inasikika redio karibia zote za jijini na tayari video ipo jikoni inapikwa, yaani ndani ya mwezi huu au mwisho wa mwezi huu lazma utaona kichupa cha AINEA Ft SHETA ndani ya SOME BODY...
 Ngoma hii imetulia na imesimama kisawasawa hasa ukisikiliza mashairi na style za uimbaji alizotumia AINEA na pia alivyopita SHETA, mwenyewe utakubaliana na mimi kuwa ngoma hii ni MOTO BALAA... nyimbo ya kwanza aliyotoka nayo AINEA inajulikana kwa jina la MOYO UTANIUMA, hii aliifanya kwa kushirikiana na mwanadada mkali kutoka UGANDA aitwaye SARA ZAWEDE, hii ilifanyika chini ya producer MAN WATER.
Baada ya hapo AINEA aliibuka na ngoma nyingine kaali itwayo SINA MPANGO NAYE, hii alishirikana na MR BLUE au KABAISA...ni ngoma ambayo ilifanya vizuri na inaendelea kufanya vizuri mpaka sasa katika redio na tv.
SINA MPANGO NAYE ilifanika chini ya producer ECK wa ECK PRODUCTION. Ngoma hii ndio ngoma ambayo ilizidi kumuinua AINEA na kumuweka katika nafasi nzuri ya kuanza kupiga show za ukweli mikoani na kwingine. Sasa imeshatambulishwa SOMEBODY ambayo ndio ngoma yake mpaya. isikilize kisha mwenyewe utaniambia kuwa AINEA NI MKALI AU SIO MKALI... ni lazima tumsifie mtu kwa kile kizuri anachokifanya...

BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU

HII NI MO DESIGN

© Copyright MO Design
Back To Top