wanafunzi wa chuo cha Uongozi wa Fedha (IFM) wakiongea na Kamanda Kova kuhusu kuongozana naye kwenda katika kituo cha polisi kigamboni ambapo waliomba ulinzi wa hosteli yao iliyopo Kigamboni lakini hawakusikilizwa,.. hii ni baada ya maandamano yaliyowafikisha mpaka mbele ya geti la jengo la Wizara ya Mambo ya ndani leo majira ya saa 4:30 asubuhi.
Hapa wanafunzi hao wa Uongozi wa Fedha (IFM) wakiwa katika maandamano kuelekea katika Ofisi za Wizara Ya Mambo ya Ndani. hii imeetokea leo majira ya saa nne na nusu asubuhi baada ya tulio lililotokea la wanafunzi kuvamiwa na majambazi na kufanyiwa kitu mbaya ikiwa ni pamoja na kuibiwa baadhi ya vitu vyao.
mashuhuda wanasema kuwa hali hii imekuwa ikijitokeza mara nyingi na wanafunzi walisharipoti matukio hayo na kuomba ulizi wa hosteli lakini polisi wamekuwa hawawasikilizi. hali hiyo ikiwa ni pamoja na tukio la leo ndio limepelekea wanafunzi hao kuamua kuandamana na kukizuia kivuko cha kigamboni mpaka pale watakapopata muafaka kutoka kwa kamanda Kova.
alipowasili maeneo hayo ya kivuko kamanda kova alikuwa akishangiliwa na wanafunzi jambo lililoonesha kuwa wanafuzi hao walikuwa na imani na kamanda Kova. alipopewa tuhuma hizo Kova aliahidi kulishughulikia Haraka iwezekanavyo.
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.