Ilikuwa ni jioni moja tulivu ambapo kijimvua cha rasharasha kilikuwa kikiendelea kunyesha taratibu, na kama kawaida ya watu wa Dar es Salaam wanavyoogopa mvua kuliko magari, alionekana mtu mmoja mmoja akipita barabarani katika mitaa ya kinondoni, watu wengi walikuwa wamejificha kwenye vibanda kusubiri kijimvua hicho kikate na wengine walikuwa tayari majumbani kwao wakijipumzisha wakati engine walikuwa ndani ya magari yao wakielekea huku na kule.
Katika moja ya mitaa ya Kinondoni ndani ya jumba moja zuri la kifahari japo lilikuwa halina ufahari wakutisha, mzee Henry Bisu alikaa na familia yake sebuleni huku wakiongea, maongezi yao yalionekana ya huzuni kidogo au tuseme kuwa ni kama kulikuwa na kutokuelewana katika kilichokuwa ninaongelewa hapo sebuleni kati ya mzee Henry Bisu na familia yake. mbali na mzee Henry Bisu alikuwepo pia mwanaye wa kwanza John Bisu, mwanaye mwengine ambaye ni Tatch Bisu na kitenda mimba chake ambaye ni Denis Bisu. mzee bisu na Mkewe Bi. Pauline walifanikiwa kupata watoto watatu wote wakiwa ni wakiume, na kwa kudra za mwenyezi mungu wote watatu walikuwa na afya njema na wote walifanikiwa kumaliza elimu ya juu kaika fani mbali mbali, ni Denis pekee ndio alikuwa bado nasoma katika moja ya vyuo vya hapa dar es salaam. wote waliishi katika jumba hilo kila mmoja akiwa na chumba chake, na hakuna kati ya watoto wote hao ambaye alikuwa tayari ameoa, wote walikuwa bado wasela pamoja na kuwa kila kukicha Mzee Bisu aliwalazimisha wanaye ambao ni John na Tatch ili watafute wake wa kuoa lakini wenyewe walipinga na kusema muda bado, kwa Denis yeye alikuwa bado na umri wa miaka 18 tu hivyo hilo swala la kuoa lilikuwa bado kabisa. maisha katika familia hiyo yalikuwa mazuri na yenye furaha kila siku, lakini siku hiyo ilikuwa tofauti kidogo kwani kulikuwa hakuna maelewano kati ya mzee Bisu na wanawe, kulikuwa na mtafarukh kidogo. badala ya kile kilichokuwa kinaendelea kila siku cha mzee Bisu kuwalazimisha wanawe watafute wake, sasa ni yeye ndio alikuwa anawaambia wanawe kuwa anataka kuoa mke mwingine jambo lililopingwa sana na wanawe hasa John.
"... Nisikilizeni kwa makini, mimi ndio mwenye maamuzi ya mwisho ndani ya nyumba hii na mimi ndio nnayepanga nini nataka kufanya sawa..." alisema mzee Bisu lakini kabla hajaendelea John alidakia.
"... hakuna anayepinga kuwa wewe ndio mwenye maamuzi humu ndani, lakini lazima uangalie, maamuzi yako hayo yatakuwa na faida gani kwetu sisi wanao pia na mama"
"... mama yenu hana cha kusema kwa vile nilishaongea naye, na nyie hili haliwahusu na halitakuwa na mazara yoyote, sana itamsaidia mama yenu kupata mtu wa kumsaidia" aliongea mzee Bisu.
"Mama hawezi kukubaliana na maamuzi hayo ya kijinga, na kama ni mtu wakumsaidia si umtafutie house girl, au kama huwezi ngoja sisi tumtafute huyo house girl na tutamlipa" alidakia Tatch kwa jazba kidogo.
"... wewe, angalia domo lako, alikuja juu mzee Bisu. unasema maamuzi yangu mimi ni yakijinga?.. kwa hiyo mimi ni mjinga si ndio?"
"... Hakuna anayesema kama wewe ni mjinga, alidakia John, ila hayo maamuzi yako sio ya busara, inavyoonesha ni kwamba umemchoka mama sasa unataka umtafutie mke mwenza bila kufikiria ni wapi ulikotoka na mama na nini kitatokea baada ya wewe kuleta huyo mwanamke humu ndani"
"... sikilizeni, aliongea mzee Bisu kwa upole kidogo, " haki ya mama yenu itabaki kuwa pale pale lakini kulingana na umri wake anahitaji apate msaidizi"
"... sisi huyo msaidizi hatumtaki humu ndani, aliongea john kwa jazba.
"tunaridhika na anachokifanya mama"
"sasa endeleeni na ubishi wenu. alifoka mzee Bisu,
"... lakini hakuna wakuyabadilisha maamuzi yangu, nilishaamua kuoa mke mwingine na lazima ntaoa basi." aliongea mzee bisu huku akiinuka na kuanza kuingia chumbani kwake.
"... sawa, we oa tu aliongea John. we kaoe huyu mwanamke wako, lakini mimi siwezi kuendelea kuvumilia haibu itakayotokea ndani ya nyumba hii, hapa kwako mimi naondoka" alimalizia John huku na yeye akiinuka.
"... Hata mimi hapa nahama", alidakia Tatch huku naye akiinuka na kuondoka. Denis yeye alikuwa kimya muda wote akiwaangalia kaka zake wakibishana na baba yao, na walipotoka na kuingia vyumbani mwao kuchukua mizigo yao na kutokomea yeye alibaki kuwakodolea macho tu. ni baada ya mama yake kutokeza chumbani alikokuwa mda wote ambapo maongezi hayo yalikuwa yakiendelea ndipo Denis alipogutuka, na kilichomgutusha ni baada ya kugundua kuwa mama yake alikuwa analia, aliinuka na kumfuata, alipomfikia alimkumbatia mama yake kisha akamuuliza kwa upole. "... mama, kuna kitu chochote ulichoongea na baba kuhusu kuoa?... ITAENDELEA JUMANNE... USIKOSE
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.