ILIPOISHIASEHEMU YA 19
Dennis akapatwa na mashaka kidogo na akawa kama anajiuliza maswali mwenyewe..."Huyu mbona nimezungumzia habari za kuingia chumbani kwake tu amekurupuka wakati alikuwa hataki kunisogelea eti kwa vile kavaa kanga moja...au kuna kitu anaficha huko chumbani nini?.."...
SASA ENDELEA NA SEHEMU YA 20
... Mawazo hayo yalipelekea Dennis kutamani kuingia chumbani kwa Hasina kuhakikisha ni kitu gani ambacho hataki kionekane huko chcumbani kwake. lakini hakufanikiwa kuingia kwani Hasina alikuwa tayari kasimama mbele yake kwa mtindo wa kama kumzuia asipite. Hata hivyo Dennis hakutaka tena kuongelea kilicho sababisha amuite Hasina, badala yake alipatwa na shauku ya kutaka kujua ni nini ambacho Hasina alikuwa akikificha chumbani kwake.
"... kwani huko chumbani kuna nini we Hasina..." alihoji Dennis akiwa amesimama sambamba na Hasina.
Hasina alijua amekwisha maana Dennis alionesha kweli kuwa na shauku ya kutaka kujua nini kipo chumbani kwake, na yeye hakutaka Dennis aingie au afahamu ni nini kilikuwa chumbani kwake, akaanza kuumiza kichwa kutafuta jinsi ya kumzuia Dennis asiingie katika chumba hicho.
"... kwani kaka Denni we si uliniita, na nilitaka nika vae ngu vizuri wewe ukaniambia nije hivyohivyo..." alionge Hasina kwa kujiamini.
"... lakini mbona nimeongelea habari za kuingia chumbani kwako ukakurupuka, kwani umeficha nini?.."
akili ya Hasina ilikuwa inafanya kazi kwa haraka na alikuwa akicheza na akili ya Dennis.
"... kaka Dennis sikiliza... mimi nimekuam,bia kuwa nilikuwa nimelala na ndio maana nimetoka jasho hivi, na hapa nilikuwa nakwenda kuoga... isitoshe kaka Denni, mimi ni mtoto wa kike na chumba cha mtoto wa kike siku zote yeye ndo anajua ni vipi anaviweka vitu vyake. kukuzuia kwangu mimi namaana kuwa kunavitu vyangu ambavyo nimeviweka vibaya na sio vizuri wewe kuviona ndio maana sipendi uingie chumbani kwangu... kidogo kama maelezo ya Hasina yalianza kumuingia Dennis maana alianza kulainika na kupunguza ukali wa maswali.
"... kwani ni vitu gani ambavyo sitakiwi kuviona?..
"... kaka denni... nafikiri unafahamu kuwa sisi wanawake na nyie wanaume tuko tofauti... na sisi wanawake kila mwezi tuna kuwa na..."
"... ahha basi sitaki kusikia habari hizo..." alimkatisha Dennis baada ya kugundua ni nini alitaka kuongea Hasina, akaamua kubadilisha mada. pia alionekana moja kwa moja kukata hata ile taamaa aliyokuwa nayo na iliyosababisha amuite Hasina pale. aliamini kuwa msichana huyo alikuwa katika siku zake kwani kauli yake ilimaanisha hivyo, hivyo hakutaka hata kugusia habari hiyo tena kwani isingewezekana kutokana na Hasina kuwa katika siku zake.
"... haya basi niambie ulichoniitia..." alihoji Hasina.
"... ah... basi ntaongea na wewe siku nyingine, we nenda kaoge..." aliongea Dennis huku akigeuza njia na kuelekea chumbani kwake. kitendo hicho kilimfurahisha sana Hasina kwani alijua kuwa tayari ameuvuka mtihani uliokuwa mbele yake. Hakuondoka pale sebuleni mpaka alipohakikisha Dennis amezama chumbani kwake na kufunga mlango na ndipo naye akatoka haraka na kurudi chumbani kwake kulitoa tatizo lililokuwa limemkabili.
Hasubuhi ya siku hiyo kaba ya mambo hayo kutokea, Mzee Bisu aliamka mapema kama kawaida yake kwa ajili ya kufanya mazoezi. lakini siku hiyo pia alikuwa hana lengo hasa la kufanya mazoezi alitamani sana kuingia tena chumbani kwa Hasina kupata ile Raha aliyoipata jana yake. alipotoka tu sebuleni akiwa na lengo la kufanya mchezo ule ule kama alioufanya jana yake, akakutana na mwanaye Dennis akiwa naye ndo anaingia pale Sebuleni kwa ajili ya kuaanza kufutilia habari mbalimbali katika televisheni, swala hilo lilimchukiza sana kwani alijuwa kuwa itakuwa vigumu kuigia chumbani kwa Hasina wakati Dennis akiwa pale, akatamani kumtimua lakini akajiuliza mwenyewe kuwa akimtimuwa mwanaye lazima atamuuliza kwa nini anamtimua, alafu yeye atamjibu nini? akajikuta tu amesimama pale sebuleni akiwa amemkodolea macho mpaka pale alipogutushwa na sauti ya Dennis.
"... Shkamoo Baba..."
"... ah,.. marahaba Dennis... eh.. vipi.. mbona mapema sana..."
alijikuta akimpachika swali bila kutarajia kulingana namsukumo uliokuwa ndani yake wa kutamani kumtimua pale sebuleni.
"... ya... kuna news nataka nizifuatilie kwenye tv ndo maana nimewahi sana leo..." alijibu dennis huku akiwa tayari anawasha luninga.
"... lakini we huoni kama utajiletea matatizo,.. kila siku unaamka mapema kiasi hiki alafu bado kulala unachelewa?.."
aliendelea kuongea mzee Bisu katika hali ya kutafuta jinsi gani amtimue Dennis ili apate upenyo wa kuingia chumbani kwa Hasina.
"... matatizo ya nini sasa baba..."alihoji Dennis akiwa tayari ameshakaa kwenye sofa kwa ajili yakuanza kufuatilia kile kilichomuamsha mapema. swali hilo kama lilikuwa gumu kidogo kwani alipojiuliza ni matatizo gani atakayoyapa kwa kuamka mapema akachemka akajikuta tu ametamka.
"... siku utadondoka ghafla, alafu watu watakushangaa... hebu rudi chumbani kalale tena kama lisaa limoja hivi ndipo uamke..."
Dennis alijikuta akigeuka kumuangalia baba yake kama alikuwa siriasi au anaongea tu, kwani kauli hiyo ya kumuambia arudi akalale tena kidogo ilimshangaza, akatamani amuulize baba yake kama alikuwa sawa, lakini alipomuangalia aligundua kuwa baba yake aliongea kabisa kutoka moyoni. ikabidi tu aikaidi kauli hiyo kwani hakuona sababu ya msingi ya kumrudisha kulala.
"... baba nilishakuambia kuna news za muhimu nataka kuzifuatilia... mi siwezi kulala tena saa hizi..."
mzee Bisu alitamani amrukie kwa vichwa lakini akasita tena na kujiuliza mwenyewe sasa nikimlazamisha si ataanza kunihoji maswali... na mimi ntamjibu nini.
akajikuta tu amekaa kimya na kumuangalia mwanaye huyo mpenda habari za asubuhi na mapema kwa jicho kali na la chuki. alikuwa amekoseshwa utamu wa siku hiyo na aliokuwa ameukusudia na kuufikiria kila wakati. akaamua kubadilisha ratiba na kwenda mazoezini lakini kichwani kwake akiwa tayari alishajiwekea mkakati atakaoufanya siku hiyo..... Ni mkakati gani?
FUATILIA SEHEMU YA 21
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.