Kumekuwa na tabia za watu kutaka kuwatapeli au kuwaibia wenzao kwa njia ya mtandao kwa kujifanya kuomba urafiki. Tabia hii imeshamiri na kukua siku baada ya siku ambapo matapeli hao pia hutumia picha za warembo wenye mvuto kutaka kuwaingiza kiulaini wanaume kwenye mitego yao.
Hua wanaanza kwa kukutumia ujumbe kwenye Facebook wakikuambia kuwa wamevutiwa na profile yako lakini cha ajabu wanakuambia kuwa uwasiliane nao kwa njia ya email ambapo hukutumia na kukuomba nawe pia utume ya kwako. mkishaanza mawasiliano anakuambia kuwa yeye ni mkimbizi yuko sehemu fulani lakini ana pesa ambazo wazazi wake walimuachia so anataka umtumie acount namba yako.
Hili lilishamtokea MO mara kadhaa lakini kwa vile alikuwa anataka kujua nini kinaendelea na nini hatima yake, aliendelea kuchat nao na kufanikiwa kutumiwa picha za warembo ili kumlainisha..
|
GRECE HORWARD katika pozi la mitego |
Huyu ndiye mrembo wa kwanza ambaye MO alitumiwa picha zake akiambiwa kuwa anaitwa GRECE HORWARD. anasema ni mkimbizi ambaye yuko Senegal na yuko kwa mchungaji wa Kanisa la CGM (jina kamili la kanisa linahifadhiwa)la mjini Dakar. Mchungaji huyo anaitwa D.... J....( majina tunayahifadhi kwa sababu maalum) na namba za simu za mchungaji huyo ni +2217766.....( zinahifadhiwa)
|
GRECE HORWARD katika pozi la mitego zaidi ili kumlainisha MO |
Binti huyu alimuambia Mo kuwa wazazi wake walipofariki waliacha pesa nyingi katika account ambayo iko katika nchi za ulaya na accounti hiyo iliandikwa kwa jina lake, na kiasi kilichomo kwenye acount hiyo ni kiasi cha dola za kimarekani Milioni 5.7. Alimuambia kuwa anataka MO amsaidie ili aweze kuzihamisha hizo pesa kwenye accounti yake kisha amtumie pesa kidogo kwa ajili ya kumsafirisha kutoka Senegal na kuja kuishi naye.
Huyu pia anaitwa RITA ADU JOHNSON. huyu pia alianza kwa kumuomba MO urafiki kupitia Facebook na kumuomba amtumie email yake ili wawasiliane kwani account yake ya facebook sio ya kudumu.
|
RITA akiwa katika pozi lenye mvuto |
|
RITA JHNSON |
RITA yeye alimuambia MO kuwa anatokea Nchini Sudan na yuko katika Kambi ya Wakimbizi Mjini Dakar - Senegal kutokana na vita vilivyotokea katika nchi yao.
akasema kuwa Baba yake Dr. Johnson Adu alikuwa Chairman Managing Director wa INDUSTRIAL COMPANY LTD Mjini Karthoum - Sudan, kabla waasi kuvamia nyumba yao asubuhi na mapema na kumuua pia na mama yake aitwaye Calaralin Adu.
Wanaonekana ni mabinti warembo sana lakini mambo yao sio mchezo, ukicheza tu unaliwa.
JAMANI JIHADHARINI NA MATAPELI WA KWENYE MTANDAO
BOFYA HAPA KWA KUJIUNGA NASI MOJA KWA MOJA NA LIKE PAGE YETU
HII NI MO DESIGN
Post a Comment
Tafadhali, Usitumie lugha ya matusi! Maoni yako ni ya muhimu sana kwetu.